Nadia Buhari
Mrembo anayeuza nyago kwenye filamu za Ghallywood, Nadia Buhari amefunguka kuwa tabia yake ya aibu inamtesa sana kiasi kwamba watu wengi wamekuwa wakimchukulia tofauti kuwa anaringa na kujisikia jambo ambalo halina ukweli wowote.
Nadia alisema; “Kiukweli aibu inanitesa. Ila watu wanatakiwa kuelewa kuwa nimezaliwa nikiwa na aibu na watu wasinichukulie tofauti, kila mtu anaasili yake.”