Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani amefariki dunia alipo kuwa akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema.
Bi Jones alizaliwa mwaka 1899
Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.
Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Alabama mwaka 1899, na amekuwa akiugua kwa siku kadha.
Mwanamke Mwitaliano, Emma Morano, ambaye ni mdogo wa umri wa Bi Jones kwa miezi kadha, sasa ndiye anayetambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi duniani.
Morano sasa ndiye mwanamke mzee zaidi duniani
Anaaminika kuwa mtu pekee duniani aliyezaliwa karne ya 19 ambaye bado yuko hai.
Source: BBC