SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Aprili 2016

T media news

YALIOJIRI UEFA





Siku ya tarehe 6/04/2016 kuanzia mida ya saa 3:45 mambo hayakua mazuri kwa baadhi ya miamba miwili ya UEFA kushindwa kudhihirisha waliokua wanasubiri wadau wengi wa mpira.





Tukianza na matokeo ya Real Madrid ilipokutana na Wolfsburg ya Ujeruman wadau wengi walitarajia kua miamba hiyo ya Dunia itaichakaza vibaya Wolfsburg na hiyo ni kutokana na matokeo ya Real Madrid dhidi ya Barcelona pale Ronaldo alipoipatia timu yake goli la ushindi ugenini na kuweza kummaliza simba aliekua akisumbua pori.




 Pamoja na hayo yote jana Ronaldo hakuweza kuonekana hata kidogo na hapo ndipo waswahili husema anaeua kwa upanga hufa kwa upanga. kilichowakuta wenzetu kwa kupokea kipigo cha goli 2 bila ni sawa na mtu kumuua Tembo halafu yeye akapigwa na mlevi. poleni sana Real Madrid.



Kwa upande wa pili matajiri walipokutana jana walionesha ulimwengu kua wote wapo vizuri na hakuna mbabe kati yao. mchezaji machachari wa PSG Zeratan alikosa penalt na kufanya matokeo ya mechi yawe 2 kwa Psg pia kwa wageni wa mechi Manchester city wakiwa na 2.

Tunasubiri marudio tuone je haliotokea jana yataendelea kutokea au laa. Tutaendelea kufahamishana zaidi yatakayo jiri katika mechi ya marudiano.