Mapenzi yanaumiza, kama hujawahi kuumia huyajui.
Na kama unahitaji ushahidi kutoka kwa mtu ajuaye maumivu yake kwanini usimuulize Idris Sultan? Ni kwasababu mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014 anauguza jeraha la moyo baada ya mwanamke ampendaye – Wema Sepetu kumchoma kwa mkuki wenye moto moyoni mwake.
Wakati akiwa safarini jijini Nairobi, alishangazwa na video inayomuonesha mpenzi wake akimbusu mwanaume mwingine. Video hiyo imekuwa viral mtandaoni. Story zinaeleza kuwa pamoja na jamaa huyo kuwa ‘chakula’, bado ni mwanaume tu na video hiyo imemuumiza mtoto wa Sultan.