SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

T media news

SHAMSA FORD 'Nilinusurika Kuaribika Ubongo na Kumpoteza Mtoto Tumboni Kutokana na Kipigo Kutoka Kwa Baba Mtoto Wangu'

Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki.

“Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa.