Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, kesho Jumatano, Aprili 06 mwaka huu anatarajia kufanya ziara wilayani Ngara mkoani Kagera, kwa ajili ya kuzindua daraja la Rusumo linalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda pamoja na jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha - (OSBP).
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habara, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honoratha Chitandaa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli na kuongeza kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imejipanga kuwasafirisha wananchi watakaokosa usafiri ili kufanikisha mapokezi.
Bi Chitanda amesema pia kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha ziara ya Rais inakwenda vizuri bila kuingiliwa na dosari yoyote inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi wote kutii sheria.
Katika ziara hiyo Rais magufuli anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakayeshirikiana naye katika Uzinduzi wa Daraja la Rusumo linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Rwanda.
Baadaye, marais hao wataelekea Kigali-Rwanda ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja.
Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.
Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.