SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 9 Aprili 2016

T media news

MATOKEO YA MAZOEA YAMEJIRUDIA TENA MECHI YA YANGA NA AL AHLY


Image result for picha za yanga za leo
                                                                                                       




Na Albogast Benjamin

Mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri umemalizika jioni hii kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

Unakumbuka msimu wa 2014? Bila shaka utakua umegundua kitu kilichotokea leo sio tofauti na kiichotokea miaka takribani miwili iliyopita.

Al Ahly na timu zingine kutoka Misri zimekuwa na jadi ya kupanga matokeo na hii si kwasababu wanabahatisha bali mipango yao inakuwa makini na mara nyingi wanafanikiwa.

Maneno mengi pasipo kufanyia kazi mapungufu

Kitu kimoja tu kilichoiponza Yanga ni kutotaka kujifunza kutokana na mechi zilizopita wakati mchezo unaanza walitakiwa kuanza kwa kasi na kuhakikisha wanatafuta bao la mapema na kutowaruhusu Ahly washambulie matokeo yake hawakufanya hivyo wakawaruhusu Ahly kuja kushambulia na wakafunga bao la mapema.

Al Ahly baada ya kutimiza malengo

Baada ya malengo ya Ahly kufanikiwa wakatulia na kucheza mpira Yanga wakazinduka na kufanya mashambulizi yaliyowasaidia kupata bao la kusawazisha baada ya mchezaji wa Ahly kujifunga. Kazi iliyofuata ni Ahly kulinda malengo yao ya kupata sare na wamefanikiwa kwenye hilo na mchezo ukawa umeisha kwa sare ya bao 1 – 1.

Kwa hakika matokeo haya si rafiki hata kidogo kwa Yanga kutokana na Historia kuibeba timu ya Al Ahly japo maneno ya soka yanasema lolote linaweza kutokea lakini uwezo nao huzingatiwa.