
Kuvaa sio jambo gumu ila shida inakuja pale ni nguo za aina gani mtu anapaswa kuvaa kulingana na mazingira na jinsi alivyo ili kuweza kuleta muonekano mzuri na wakuvutia katika jamii inayotuzunguka, wataalamu wa mambo ya mitindo wanawaelezea wanawake kama ni watu wanaopenda sana kuvaa na kupendeza japokuwa sio wote ila kwa asilimia kubwa wanajitaidi kwenye kutupia halikadhalika na wanaume.
Leo nimekuletea aina kumi za mitupio a.k.a nguo za jinsia ya kiume ambazo hupendwa zaidi na wanawake endapo zikivaliwa kwa ufasaha na kufuata taratibu zote, hivyo usije ukashangaa siku ukiwa umevaa moja wapo ya mavazi haya ukawa unaangaliwa sana na watu wenye jinsia ya kike, unaweza ukatazama hapa chini na kujifunza taratibu jinsi ya kutengeza muonekano mzuri kwa kutumia mavazi haya.







