SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Aprili 2016

T media news

Kinachoendelea Afrika ya Kusini na Kiwe Funzo Kwa Nchi za Bara la Africa...Rais Afikishwa Mahakamani....

Kinachoendelea Africa ya Kusini na kiwe funzo kwa nchi za Bara la Africa,Huenda karata ya upinzani ya Nchi hiyo isifanikiwe kwasasa,ila Ilifanikiwa hapo awali baada ya kumpeleka Rais Mahakamani na Upinzani kuibuka kidedea.

Taifa langu Tanzanzia tunahitaji katiba mpya itakayoruhusu Rais kupandishwa kizimbani kwa kutumia mamlaka vibaya (Kufuja mali za umma) mambo ya kuwafanya marais kuwa ni watu wasiyogusika ni mambo ya kikoloni sana.
Tuitafuteni haki ya kupata katiba mpya itakayo wawajibisha Marais ama wakiwa madarakani ama nje ya Madaraka.

Vile vile tuwe na Katiba itakayomfanya Rais kuwepo bungeni na siyo utaratibu wa Sasa Wa Rais kulihutubia Bunge kisha mambo mengine yote anamuachia Waziri mkuu, Hapa hatuwafanyii Wananchi mazuri,Kumbuka Waziri huyu alichaguliwa na jimbo moja sasa anakuja kujibu Maswali ya nchi nzima....Tubadili muelekeo wa kisiasa kama tunataka kuwaletea Watanzania maendeleo na siyo maigizo ya kisiasa.

Kwasasa ni lazima waliyopo madarakani mkubali kupoteza vitu fulani na kuongeza vitu fulani vyenye manufaa kwa Wananchi....
TUITAFUTENI KATIBA MPYA