SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 6 Machi 2016

T media news

Waitifaki wa Israel wameitaja Hizbullah kuwa kundi la kigaidi

Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amesema waitifaki wa utawala haramu wa Israel ndio wallioitaja harakati ya muqawama ya Hizbullah kuwa kundi la kigaidi.Brigadier Jenerali Yadollah Javani, mshauri wa mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema wale ambao wameibua mgogoro Syria na wanaounga mkono utawala wa Kizyauni wa Israel ndio walioitaja harakati ya mapambano ya Hizbullah kuwa kundi la kigaidi.Javani amesema hatua ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ya kuituhumu Hezbollah ni hatua ya kujidhuru na ni kosa la kistratijia litakalolipotezea itibari baraza hilo.Amesisitiza kuwa Hzibullah ni harakati mashuhuri ambayo iliundwa kwa ajili ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel, kulinda ardhi ya Lebanon na kutetea haki za Waislamu.Kamanda huyo wa kijeshi nchini Iran amesema hatua ya tawala za Kifalme katika Ghuba ya Uajemi kuitaja Hizbullah kuwa kundi la kigaidi ni ishara kuwa nchi hizo za Kiarabu zinafuata nyayo za Wazayuni kwa lengo la kutekeleza matakwa ya Marekani.Brigadier Jenerali Yadollah Javani amesema Hizbullah ni harakati inayoheshimika katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba ina nafasi ya kipekee miongoni mwa mataifa ya Waislamu na Waarabu.