SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 6 Machi 2016

T media news

Kampeni za uchaguzi wa rais Congo Brazzaville

Wagombea tisa wa kiti cha urais huko Jamhuri ya Kongo wameanza kampeni zao za kuwania kiti cha urais.Uchaguzi wa rasi Congo Brazzaville umepangwa kufanyika tarehe 21 machi na Ijumaa wagombea walianza kutembelea maeneo ya nchi hiyo kujinadi.Rais wa sasa Denis Sassou Nguesso anatetea nafasi yake hiyo huku akiwa na matumaini kushinda katika duru ya kwanza. Hata hivyo wapinzani wanasema hiyo ni ndoto kwani kuna mashindano makali na ni vigumu mshindi kupatikana katika duru ya kwanza. Aidha baadhi ya wapinzani wametilia shaka kuwa huru na wa haki uchaguzi huo.Mgombea mwandamizi wa upinzani Tsaty Pascal Mabiala wa chama cha Pan-African Union for Social Democracy, UPADS ameanzia kampeni zake kaskazini mwa nchi.Wapinzani aidha wanasema hatua ya Sassou Nguesso kuwania urais kwa mara ya tatu mfululizo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.Tarehe 15 Oktoba mwaka jana, kulifanyika kura ya maoni Congo Brazzaville kuhusu mabadiliko ya katiba kwa lengo la kumruhusu Sassou Nguesso awanie tena urais.