SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 21 Machi 2016

T media news

Jaguar kufanya kolabo na Nicki Minaj

Msanii Jaguar kutoka nchini Kenya amefunguka kuhusu collabo na Nicki Minaj baada ya kuona show yake Afrika Kusini.

Wakenya wachache wamesafiri kwenda Afrika Kusini weekend hii kwaajili ya show ya rapa Nicki Minaj ya ziara yake ya Pink Print mjini Johannesburg.

Jaguar amekuwa miongoni mwa watu waliokwenda Afrika Kusini kwenye show hiyo na kufanya video pia.

Ripota wa habari za burudani alikutana na Jaguar baada ya kutoka Afrika Kusini na kutaka kujua kama kuna collabo inakuja na Nicki Minaj au lah?

Jaguar alisema “Ni msanii mbunifu na aliyeogopa kuthubutu, kuna kitu kila msanii anaweza kujifunza kutoka kwa msanii mwenzake na mambo kama haya ndiyo husababisha collabo” Jaguar alisema hayo baada ya kutoka Afrika Kusini.

Jaguar na mwanamitindo kutoka Nairobi Pendo Small walihudhuria show hiyo.