SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 6 Machi 2016

T media news

Buhari: Kutegemea mafuta kumevuruga uchumi wa Nigeria

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema kutegemea kupita kiasi pato la mafuta ya petroli ni chanzo kikuu cha matatizo ya kiuchumi nchini humo.Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, Buhari amesema Nigeria imejisababishia matatizo ya sasa ya kiuchumi kwa kutegemea pato la mafuta na kuongeza kuwa serikali zilizopita ndizo zinazopaswa kulaumiwa kwa hali hiyo.Matamshi ya Buhari yamekuja baada ya Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta ya petroli Afrika na uchumi mkubwa zaidi barani humo, kukumbwa na matatizo chungu nzima kutokana na kuporomoka bei ya mafuta katika soko la dunia katika kipindi cha mwaka mmoja.Buhari ameongeza kuwa Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani OPEC inapaswa kushirikiana ili kujadili hali ya hivi sasa katika soko la mafuta duniani.Alhamisi iliyopita, waziri mdogo wa mafuta Nigeria alisema baadhi ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani, Russia ikiwemo, zinatazamiwa kukutana Moscow Machi 20 ili kujadili njia za kukabiliana na kuporomoka bei ya mafuta.