SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

Polisi ya Burundi yamtia mbaroni kiongozi wa upinzani

Polisi nchini Burundi imetangaza kuwa, imemtia mbaroni kiongozi mmoja wa chama cha upinzani.Hugo Haramategeko mkuu wa chama kinachoipinga serikali cha Umoja kwa ajili ya Ustawi wa Burundi (NADEBU) ametiwa mbaroni katika eneo la Mutakura linalotajwa kuwa na upinzani mkubwa dhidi ya serikali ya Rais Pierre Nkurunziza, jijini Bujumbura.Hata hivyo polisi hawajatoa maelezo yoyote kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Haramategeko.Hii ni katika hali ambayo tangu mwezi April mwaka jana wakati Rais Nkurunziza alipotangazwa na chama chake cha CNDD-FDD kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo katika uchaguzi uliopita, nchi hiyo ndogo ya katikati mwa Afrika imekuwa likishuhudia machafuko ambayo yamegharimu maisha ya mamia ya watu huku maelfu ya wengine wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao.Jamii ya kimataifa imetaka kufanyike mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na vyama vya upinzani kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa nchi hiyo.