SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Machi 2016

T media news

NEYO NA DIAMOND PLATNUMZ KUPANDA JUKWAA MOJA JIJINI MWANZA

Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Ne-yo athibisha ujio wake nchini  Tanzania katika tamasha kubwa la Jembeka Festivallitakalofanyika jijini Mwanza mwezi Mei mwaka huu.




Kupitia ukurasa wao Jembe ni Jembe ambao ndio haswa watayarishaji wa shoo hiyo wameandika hivi “Ne-yo &Dimond Platnumz live at the Grand Jembeka Festival,usikose show hii ya kihistoria mwanza 21/05/2016 kwa Tsh 10,000”

Katika Shoo hiyo atakuwepo pia Diamond Platnumz ambapo nae kwa sasa yupo katika ‘tour’ yake ulaya.


Kumbuka wawili hao wako katika matayarisho ya ngoma yao ambapo Diamond amemshirikisha Ne-yo, kwamujibu wa Diamond Platnumz alisema video yake itafanyikia ulaya na Afrika.