SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 21 Machi 2016

T media news

Millen Magese: Tanzania Hainisupport Kwenye Kampeni Zangu za Endometriosis..Siwezi Poteza Muda....


Ukweli mchungu na kuusema ni muhimu ili wahusika wajirekebishe. Millen Magese yupo kwenye kampeni kubwa dhidi ya ugonjwa unaowatesa wanawake wengi duniani akiwemo yeye, Endometriosis ambayo kwa sasa inapewa support dunia nzima.

Na wikiendi iliyoisha alifanya matembezi nchini Afrika Kusini ya kampeni nyingine aliyoipa jina #13IsEnoughFindCure4Endo inayosisitiza umuhimu wa kupatikana kwa tiba hiyo. Lakini Miss Tanzania huyo wa zamani, amedai kuwa Tanzania imeshindwa kumuunga mkono. Anadai kuwa Watanzania wamekuwa wakisupport pale tu anaposhinda kitu.


Aliamua kuusema ukweli huo baada ya mrembo mwenzie, Miriam Odemba kumpongeza na kumshauri afanye matembezi kama hayo Tanzania pia.

Ni kweli, ni muda sahihi wa Tanzania kumuunga mkono Millen kwenye juhudi zake hizo za kutafuta tiba ya ugonjwa huo uliomfanya afanyiwe upasuaji mara 13.