KISUKARI NI NINI?
Katika miili yetu kuna mfumo tata wa mishipa ya damu tunayoweza kuichukulia kama mabomba yenye ukubwa kuanzia inchi moja (sentimita 2.5) hadi madogo kabisa ya inchi 0.0002, kiasi cha kutosha cha kupitisha chembe moja tu nyeupe kwa wakati mmoja. Damu husafirisha virutubisho vyote vinavyohitajika na kila seli katika mwili wako ili ifanye kazi sawasawa. Chanzo cha nishati kwa ajili ya seli ni sukari sahili inayoitwa glucose. Glucose (sukari) nyingi kupita kiasi inaweza kuziharibu seli. Kwa hiyo una njia ya ajabu na kurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Hufanya hivyo kwa kutumia insulin, kitu kitolewacho na seli zilizo katika kongosho.
Kisukari ni ugonjwa sugu ambapo kiasi cha sukari kinachosafirishwa na damu hakirekebishwi kama ipasavyo. Ama mwili hauzalishi insulin kawaida (kisukari namba 1 kinachojulikana pia kama T1DM, au T2DM). Aina ya tatu ya kisukari inaweza kutokea kwa wanawake wajawazito ambao waliwahi kuwa na kisukari kabla. Mara nyingi hutokea baada ya miezi mitatu ya ujauzito. Unene uliokithiri wakati wa mimba ni chanzo kikubwa cha unene uliokithiri kwa watoto. Pia huongeza uwezekano wa shinikizo kubwa la damu wakati wa mimba, na matatizo mengine ya ujauzito. Watoto wanaozaliwa na akina mama wanene kupita kiasi wana hatari zaidi ya kuwa na dosari za kuzaliwa na matatizo ya moyo.
Kisukari wakati wa mimba kinaweza kusababisha matatizo makubwa kwa mama na mtoto. Kiwango kikubwa cha sukari wakati wa uzazi huathiri utendaji kazi wa seli za mtoto, jambo linalosababisha kufa kwa seli na kuongezeka kwa kasoro kwa mtoto.
Watu wenye kisukari mara nyingi hulalamika kuwa wanakojoa sana. Kiwango kikubwa cha sukari katika damu huongeza mkojo. Ongezeko la upungufu wa majimaji (na sukari) kwa njia ya mkojo huleta kiu na kuwasababisha kunywa maji mengi kujazia. Uzito unaweza kupungua, na uharibifu wa kudumu wa neva na mishipa ya damu unaweza kutokea. (uharibifu wa mishipa ya damu unaweza kuleta ugonjwa wa moyo, kiharusi, na figo kushindwa kufanya kazi). Kuharibika kwa mishipa ya damu iliyoachiwa inaweza kusababisha kukatwa kwa viungo.