Wanasema ni vyema kusambaza habari njema zaidi na zinazoongeza hasira kwa vijana kupambana kuliko vinginevyo, na huenda hili likawa moja kati ya faida za kuonesha ulichonacho kwenye mtandao wa kijamii (inspiration).
Msanii wa kike wa Bongo Fleva ambaye sio mkongwe kwenye game, Malaika aliyesikika na wengi kwa mara ya kwanza kwenye wimbo wa ‘Uswazi Take Away’ akishirikishwa na Chege, huenda akawa ndiye msanii wa Bongo Fleva anayemiliki mkoko wa gharama zaidi nchini kwa zilizowahi kuoneshwa.
Mrembo huyo anasukuma Range Rover Mpyaa (chukua muda kujua model yake) iliyoingia mjini hivi karibuni na ikipaki unaweza kuiona taswira ya mkwanja mrefu.
Picha ya gari hilo la kifahari imewekwa Instagram na Mtayarishaji wa video, Hanscana.
“Sasa Malaika… huku ni kukomoana, hakika wewe ni mwanamke wa nguvu,” aliandika Hanscana kwenye picha hizo.