SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 25 Machi 2016

T media news

Ash-Shabab 156 watiwa mbaroni na polisi ya Somalia


Ash-Shabab 156 watiwa mbaroni na polisi ya Somalia
Polisi ya Somalia imetangaza kuwatia mbaroni watu 156 kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la ash-Shabab. Kwa mujibu wa polisi ya nchi hiyo, watu hao wametiwa nguvuni katika jimbo la Puntland kaskazini mwa Somalia.
Afisa mmoja wa polisi wa nchi hiyo anayejulikana kwa jina la Abdul-Hakim Yusuf Hussein amesema kuwa, watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni kali iliyofanywa na maafisa usalama mjini wa Puntland. Ameongeza kuwa, wanachama hao wa ash-Shabab wametiwa mbaroni katika maeneo tofauti ikiwemo mahotelini, vijijini, katika vituo vya upekuzi na maeneo mengine mbalimbali. Kamanda Hussein amesema kuwa, usaili waliofanyiwa ndio umebainisha kuwa watu hao ni wanachama wa kundi hilo la kitakfiri ambalo limekuwa likitenda jinai ndani na nje ya mipaka ya Somalia. Hadi sasa zaidi ya wanachama 70 wa kundi la ash-Shabab wameuawa na makumi ya wengine kutiwa mbaroni, katika operesheni za polisi ya Somalia zilizoanza wiki iliyopita katika mji wa Puntland. Mapigano baina ya jeshi la Somalia na wanamgambo wa ash-Shabab yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.