Ukweli wa kushangaza juu ya Mbu:
Simulizi ya Qurani dhidi ya mbu ambayo ni tofauti sana na ile ya wanyama wengine wote. Ni mdudu pekee ambaye ametajwa kwa kukanusha kwa msisitizo kwamba kuumbwa kwake kunaweza kuleta sababu yoyote ya aibu kwa Muumba wake.
Hivyo ndivyo Quran inavyosema:
“Mwenyezi Mungu haoni haya (au haya) kutaja mfano wa mbu kwa sababu ya kile kinachobebwa juu yake . . . ”
Kama katika aya hizi, alipotaja majina ya wadudu wadogo kama inzi na buibui, na akasimulia mifano kuwahusu, waabudu masanamu walianza kupinga.
Walidhani wameipata fursa waliyokuwa wakiitafuta ili kuidhalilisha Quran. Je, Mwenyezi Mungu angewezaje kusema kuhusu mambo madogo na yasiyo na maana kama haya? Je, inaweza kuwaje duniani? Mwenyezi Mungu Mtukufu alijibu pingamizi zao kwa aya ya 26 ya surat Al-Baqara:
إِنَّ اللَّهَ لَا يَسْتَحْيِي أَنْ يَضْرِبَ مَثَلًا مَا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ
Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu, Al bakarah 26.
Mbu wa Kike aliyekomaa kiumbe huyu mdogo ametolewa kama mfano katika Qur'ani Tukufu ili kuonyesha jinsi alivyo na asili ngumu sana!
WANA SAYANSI WA KARNE YA 21 WAMEFANYA UTAFITI WA KINA UNAO MUHUSU MBU BAADA YA KUONA MDUDU HUYO AKIZUNGUZWA NA MWENYEZI MUNGU KATIKA QUR'AN WAKABAINI HAYA YA FUATAYO:
1- Mbu.
2- Ana macho mia moja kichwani.
3- Ana meno 48 mdomoni.
4- Ndani ya mwili wake mdogo kuna Nyoyo tatu kamili!!..
5- Ana visu sita katika pua yake na kila kisu kina matumizi yake maalum.
6- Ana mbawa tatu kila upande.
7- Katika mwili wa mdudu huyu kuna mashine ya kidigitali ya X-RAY..Inaitumia kutofautisha ngozi ya binadamu kwenye giza katika rangi ya violet.
8- Mwili wake pia una chanjo ndogo inayofanya kazi ya ganzi ya kienyeji ili kumsaidia kuingiza miiba yake kwenye ngozi ya binadamu bila kuhisi au maumivu yoyote yatokanayo na kunyonywa kwa damu.!!!
9- Ana chombo cha kupima damu, kwa sababu haipendi aina zote za damu…!!!
10- Ana utaratibu maalum wa kuharakisha mtiririko wa damu ili iweze kuivuta haraka.
Na ugunduzi wa ajabu zaidi wa Sayansi ya Kisasa ni kwamba kuna Mdudu mwingine mdogo sana wa Microscopic anayeishi juu ya Mbu huyu Kazi ya Mdudu huyo Alie juu ya Mbu hung'ata Mbu afe mapema Ndani ya Siku tatu. Lau Allaah Asingemueka Mdudu huyo juu ya Mbu basi Mbu wangeweza ishi zaidi ya Siku 3 na kuleta madhara Makubwa mno.
KATIKA KUMSOMA MDUDU MBU NDANI YA QUR'AN TUNAPATA MAZINGATIO MAKUBWA MNO.
Kwa utukufu wa Allaah namna alivyo ishusha Qur'an Aya Moja tu ya Qur'an inatoa Vitabu 100 Iwapo itachambuliwa Kwa kina Aya hiyo
Unadhani hawa Wana Sayansi kilicho wasukuma kumjua Mbu Walikurupuka ? Laa walitaka kufahamu ukweli wa MWENYEZI MUNGU Katika alivyo viumba
Na ndio maana ALLAH kwa kusema:
“Kwa mfano Mbu na kilicho juu yake…!!!” Sidhani kama wengi mlikua mnafahamu juu ya Mdudu mdogo kama Mbu anaweza kua na Kiumbe kingine juu yake Chenye Kazi maalum.
Hi ndo Qur an bwana wee Endelea kuidharau Tu Ila Ukweli utabaki pale pale Quran ndo kitabu cha Haki kisicho na Shaka Ndani yake
Makala hi Imeandaliwa na Mimi
Al Habib CHOTARA MWEUSI SULTAN
wabillaahi Tawfiq Wah Adhaah Asalam Aleykum warahmah Tullaah barakatuh.
Usisahu ku Share Islamic News na wengine wanufaike.