SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 10 Oktoba 2021

T media news

KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

 



KISA ICHI KIMEKUSANYWA  NA KUANDALIWA VEMA NA TAWFIQ MASSINI.




      KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

              SEHEMU YA KWANZA

Ni kisa cha  hidhri ameelezewa kama Nabii au Walii au hata Malaika aliye ahi mpaka leo hii ni nabii ambaye bila ya musa uwenda tusinge mfaham

ALLAH natusimlia katika qurani  sura ya 18 aya 60 mpaka 82

"Nakumbukeni musa alipomwambia kijana wake  nitaendelea na safari  mpaka  nifike katikati ya  maungano ya bahari mbili  au niendele karne na  karne mpaka  nikutane na huyo ninayetaka kukutana  naye."

Kabula ya kisa cha hidhiri tuanze kisa cha musa nacho kwa uchache........

...Nabii Musa A.S. alipokuwa mkubwa, mkewe Firauni alimwamrisha mama yake amlete ili apate kuishi katika jumba la Firauni. Alipomleta akamchukua mpaka kwenye chumba cha Firauni akamweka hapo ili acheze naye Firauni. Siku moja Nabii Musa A.S. alipokuwa akicheza na Firauni, akanyoosha mkono wake mpaka kwenye ndevu za Firauni akazivuta kwa nguvu hadi akazikata baadhi yake. Firauni aliwaambiya watu waliokuwa naye: “Jee, hamuoni afanyavyo mtoto huyu? Bila shaka huyu mtoto ni adui yangu!” Firauni akamtuma Musa kwa wachinjaji ili kusudi wamchinje, Bibi Asia mke wa Firauni akasikia khabari hii akaja mbio mbio kwa Firauni akasema: “Jee, imekuijia nini hadi ukabadili rai yako uliyoniahidi?” Firauni akamjibu: “Hukumuona vipi jinsi anavyofanya! Anataka kupigana na mimi?” Asia akasema: “Tumjaribu kwa jambo tupate kujua haki, leta makaa mawili ya moto na shanga mbili, ikiwa atachukua shanga utajua ya kwamba ana akili, na ikiwa atachukua kaa la moto utajua kuwa yeye hana akili ni mtoto mdogo, anacheza na kufurahi kama desturi ya watoto wadogo wengine walivyo.” Kwa hivyo, wakaleta wakaweka mbele ya Nabii Musa A.S. shanga mbili na makaa mawili ya moto, Nabii Musa A.S. akanyoosha mkono wake moja kwa moja kutaka kuchukua ushanga lakini Malaika Jibril A.S.

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 2

     KISA CHA NQBII MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 2

....Akaubadili mkono wa Nabii Musa A.S. na kuuelekeza kwenye kaa la moto kisha akalichukua mpaka mdomoni mwake likaunguza ulimi wake. Na inasemekana hii ndio ilikuwa sababu iliyomfanya Nabii Musa A.S. asiweze kusema vizuri. Bibi Asia akasema: “Jee, huoni kitendo chake? Hakika yeye ni mtoto asiye na akili.” Kwa hivyo Firauni alipoona ukweli wa mambo yalivyo akamwachia huru hakumuua. Na Mwenyezi Mungu S.W.T. kampigia mfano mzuri Bibi Asia mke wa Firauni katika Surat Tahrym aya ya 11

KISA CHA MKE WA FIRAUN

Mke wa Firaun alikuwa akiitwa  ASYA BINT MUZAAHIM. Allah (subhanahu wataala) Amemtaja Bibi Asya (radhi za Allah ziwe juu yake) kwenye Quraan bila ya kulitaja jina lake ndani ya Suratu Tahrim aya ya 11 pale aliposema “Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.”

Ni mwanamke wa namna gani hadi Allah (subhanahu wataala) amtaje katika Quraan? Kama tulivyoeleza huyu alikuwa ni mke wa Firaun.Firaun ambae alipewa na Allah neema ya utajiri na nguvu katika wakati wake.Firaun ni yeye alikuwa na maamuzi  juu ya kila kitu kwa wana wa israil. Ilifikia hatua akawaambia watu wake “Simjui Mungu yeyote kwa ajili yenu ila Mimi” Allah anatueleza ndani ya Quraan pale aliposema “Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa”(79:24).Firaun alikufuru kwa hali ya juu kabisa na akaadhibiwa na Allah.Kisa chake tunakijua ni maarufu.

Asya (radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ndie malkia ndani ya

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 3

KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 3

....Kasri la Firaun na alimiliki kila aina ya mapambo mazuri,vijakazi na alipata kila kitu alichokitaka katika hali ya juu kabisa pia aliloliridhia ndio lililokuwa linafanyika katika kasri hiyo.Allah anatupa mfano wa mwanamke huyu,ambae kwa dunia ya sasa angekuwa ni mwanamke tajiri na mwenye nguvu sana  kuliko wanawake wote katika uso wa dunia hii.Sasa  ni kwa nini Allah (subhanahu wataala) amemtaja mwanamke huyu kama mfano katika Quran?
Asya (radhi za Allah ziwe juu yake) alimuamini Nabii Mussa (alayhi ssalam) na akuifuata dini aliyokuja kulinganiwa na Nabii Mussa (alayhi ssalaam) ambayo ni uislamu kwa siri. Firaun alipo gundua hilo alimkabili Bibi Asya na kumuuliza juu ya jambo hilo,kwa ushujaa kabisa Bibi  Asya (radhi za Allah ziwe juu yake) alikubali kuwa yeye anamuamini Allah ambae ndie mungu wa Mussa (alayhi ssalaam). Basi Firaun aliita majeshi yake na akamleta Bibi Asya kisha akawa anamuadhibu sana,kwa kumpiga hadi kumtoa damu ili tu aache hii dini ya Mussa (alayhi ssalaam). Lakini firaun hakufanikiwa kwa hilo juu ya mateso aliyompa. Asya (radhi za Allah ziwe juu yake) kwa rehma za Allah (subhanahu wataala) alikuwa na msimamo kabisa  na

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 4

KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 4

....Imani yake na hakubadili msimamo huo licha ya adhabu zote alizopata kutoka kwa Firauni.Kuna Hadith zinatueleza ya kuwa Firaun alimfunga Bibi Asya maziwa yake kwa minyororo kisha akamning’iniza kwenye dari, alilia sana Asya kwa maaumivu kisha akasema kumwambia Allah maneno ambayo yamo ndani ya Suratu Tahrim aya ya 11 “….., alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.”
Na Allah (subhanahu wataala) hapo hapo alimuonyesha Bibi Asya  makazi yake ya peponi. Kuna baadhi ya mapokezi  yanasema kuwa Bibi Asya  akawa anatabasam baada ya kuona makazi yake peponi,jambo hili lilimshangaza Firaun na akawa anauliza,vipi huyu anatabasam katika adhabu kali kama hii nilompa ya kumfunga na minyororo maziwa yake juu ya dari?Lakin ni Allah (subhanahu wataala) ambae alimfariji mja wake huyu kwa kumuonesha makazi yake mazuri kabisa peponi na ndipo akatabasam na akafa hali ya kuwa
amening’inizwa kwenye dari.

Mapokezi mengine 
Inasemekana aliuawa na Firauni kwa kumtupia jiwe kubwa alipokataa kubadili dini ya Nabii Musa A.S. na badala yake amuabudu Firauni.

  Juu ya utukufu aliokuwa nao lakini hakujali alijua kuwa ni vya mpito na huko akhera ndiko kwenye makaazi ya kudumu na kwenye starehe kwa waja wema.

Allah (subhanahu wataala) anatufahamisha ya kwamba dunia hii kila alichokupa kiwe kizuri vipi lakini abadan hakiwezi kufikia hata kidogo yale yaliyopo Jannah.Hakuwa tayari kuuza dini yake kwa ajili ya dunia.

Tupate mafunzo kutoka kwenye kisa hichi tusiwe tayari kuuza dini yetu na akhera yetu kwa sababu ya maisha ya dunia na tuwe na misimamo juu ya uislamu wetu.Hayakuwa maisha ya dunia ila ni starehe za mpito.

Suratul Hadid aya ya 20 Allah anasema “Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto.

Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi.

Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.”
Allah atujaalie kuwa wale wenye kupata mazingatio na kuyafanyia kazi.Na atupe msimamo ndani ya dini yetu.Na atujaalie tuipate pepo yake kwa rehma zake.Aaamin.

 ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 5

KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 5

....tu alipoteuliwa kuwa Mtume, Mussa hakuanza kwa kufanya yale mambo ambayo sisi hivi leo huyaona kuwa ndio dini yaani kama vile kuswali, kufunga, kutoa zaka na kadhalika. Bali jukumu la awali alilopewa ni lile la kwenda Ikulu kumkabili Firauni aliyekuwa akitawala kidhalimu. 

"...Wakumbushe watu Mola wako alipomwita Musa, akamwambia nenda kwa wale watu madhalimu. (26:10) Na kwa yakini tulimtuma Musa kwa Firauni na Hamana na Karuni (40:24) Nenda kwa Firauni. Bila shaka yeye amepindukia mipaka (20:24) Nendeni kwa Firauni kwa hakika amepindukia mipaka (20:43) 

Kwa mujibu wa aya zote hizo, ni sahihi kusema kuwa Nabii Musa alianza kazi ya Utume kisiasa, kwa sababu hicho alichokifanya ndicho kinachofanywa na wanasiasa wa upinzani hivi leo, tofauti tu ni kwamba yeye alifanya hivyo kwa muongozo wa Mwenyezi Mungu. Kwa maana hiyo basi, wanadini ambao ndio warithi wa Mitume ndio wanaopaswa kubeba jukumu alilobeba Musa.

Kabla ya kwenda kwa Firauni, kwanza Musa aliomba apewe msaidizi wa kumsaidia katika uzungumzaji. Akamteua 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 6

KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 6

....Haruni ambaye kwa mujibu wa historia alikuwa mzungumzaji hodari na mzoefu wa masuala ya kisiasa.

Wote wawili wakamwendea Firauni. Baada ya kujitambulisha kwake kuwa wao ni Mitume wa Mola wake na kumfikishia ujumbe waliopewa kuwa awaachie huru wana wa Israili na asiwatese, Firauni akauliza "huyo Mola wenu ni nani? (20:49) 

Firauni aliuliza swali hilo kwa sababu yeye mwenyewe pia alijiita mungu, Na 'uungu' huo ndio uliokuwa msingi wa utawala wake wa kisiasa, Kwa kuuliza swali hilo, lengo lake hasa lilikuwa ni kutaka kujua mtazamo wa Musa juu ya madaraka yake. Kwa hiyo jibu la Musa lingemwezesha kung'amua mwelekeo wa Utume wake katika siasa za Misri. Musa alipozieleza sifa za Mungu Muumba ambaye ndiye anayestahili kuabudiwa na kuogopwa, Firauni akauliza swali lingine kuwa kama yeye Musa alipewa ujumbe ule katika kipindi kile, vipi basi kuhusu watu wa karne zilizopita ambao hawakuishi kwa mujibu wa ujumbe huo. (20:5) 

Firauni aliuliza swali hili la pili kimtego. Yeye tayari alikuwa na jawabu kuwa, kwa karne nyingi wazee wao walikuwa wakiabudu miungu bandia isipokuwa alitaka tu Musa ajibu kuwa wazee wao walipotea kutokana na jibu hilo, Firauni angeyateka mazingatio ya watu wake kwamba, badala ya akili zao kutafakari hoja nzito za Musa zifikirie matamshi ya Musa dhidi ya wazee wao. Kwa mbinu hiyo, alitaraji angemmaliza Musa mapema ili ule ujumbe wake usipate kusambaa nchini, kwani ingepatikana hoja ya kusambazia propaganda kuwa Musa amewakebehi 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 7

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 7

....Wazee wao. Mbinu kama hizi mara nyingi zimetumika kuwahadaa watu wenye upeo mdogo wa kufikiri, Hata wapinzani wa Mtume Muhammad, Makka walitumia mbinu za aina hiyo. 

Lakini kinyume na matarajio ya Firauni, kwa hekima, Musa alijibu kuwa habari za watu hao wa zamani anazijua Mwenyezi Mungu ambaye ana rekodi ya kila jambo katika kitabu chake na hana udhaifu wa kupoteza kumbukumbu. (20:52) Kama Musa angejibu kuwa watu hao wa zamani walikuwa wapotevu na hivyo watakuwa kuni za Jahanamu lingemsaidia Firauni kufikia lile lengo lake alilokuwa nalo kichwani wakati alipoulizwa swali. Baada ya jibu la Musa kumvurugia shabaha yake, Firauni sasa akamtaka Musa atoe hoja za kuthibitisha ukweli wa madai yake (7:106). Ndipo Musa alipoonesha miujiza, Kwanza alitupa fimbo yake ambayo iligeuka nyoka (7:107) na kisha akatoa mkono wake ambao ulikuwa unang'ara (7:108). 

Kuona miujiza hiyo, Firauni akachanganyikiwa na kuuliza kwa hamaki, "kumbe wewe Musa umekuja kututoa nchini mwetu kwa nguvu za uchawi wako (20:57). Hapa Firauni alitumia mbinu nyingine ya kujinusuru na hatari ya Musa. Badala ya kusema, umetujia na miujiza, yeye akasema umetujia na uchawi. Lengo lake lilelile la kuvuruga 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 8

      KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                     SEHEMU YA 8

....mazingatio ya watu waliokuwa wakitazama kwamba waione ile miujiza kama uchawi tu ambao hata watu wengine wa kawaida wengeweza kuufanya. Kwa mbinu hiyo, angevunjilia mbali hoja ya ile ya miujiza ambayo ingethibitisha utume wa Musa na hivyo kuwafanya watu wamkubali Mungu aliyemtuma mtume huyo jambo ambalo lingeshusha hadhi ya 'uungu' ya Firauni na kumpotezea nguvu zake za kisiasa na hatimaye madaraka yake. 

Ifahamike kuwa, Firauni alikwishabaini kuwa Musa alikuwa na dalili za Utume, kwa maana hiyo, alikwishadhihirikiwa na ukweli wa yale yote aliyokuwa akiyasema Musa. Lakini alikuwa anakwepa kukiri kwa hofu ya kupoteza ufalme wake.

Maelezo ya historia ya Musa katika Qur'an inaonesha kuwa Musa alipelekwa kwa wakuu wa Misri yaani Firauni, Amana na Karuni akiwa na muelekeo wa wazi wa kupiku mamlaka yao yaliyosimamia juu ya msingi wa dhana ya uungu bandia.

Kwanza, kule kujitokeza kwa Musa mbele yao bila hofu licha ya kukabiliwa na jinai ya kuua mtu wa Taifa la Firauni. Musa alilazimika kukimbilia nchi nyingine kujificha baada ya Firauni kutoa amri akamatwe. 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 9

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 9

.....Sasa iweje mtu huyo aibuke na kwenda moja kwa moja Ikulu si kwa minajili ya kuomba msamaha bali kwa lengo la kumtaka Rais na Mawaziri wake wamtambue kuwa yeye ni Mtume wa Mungu Muumba wa ulimwengu na kwamba wao watawala waache sheria na kanuni au sera zao na badala yake wafanye vile atakavyo Mungu. 

Ujasiri huo tu ulitosha kuwa ishara ya utume wa Musa. Isingelikuwa rahisi kwa mtu wa kawaida tena basi mwenye hatia ya mauaji kuwakabili watawala namna hiyo. Isitoshe taifa la Musa lilikuwa dhaifu au tuseme nyonge chini ya utumwa hivyo hatakama Musa angekamatwa na kuhukumiwa kifo, lisingeweza kumtetea kwa namna yoyote ile. Na huenda baadhi yao wangemlaumu kwa jaribio hilo hatari! 

Kwa hali hiyo, hata kabla ya kuonesha miujiza, Firauni na watu wake walikwishagundua kuwa Musa alikuwa na nguvu fulani kubwa nyuma yake iliyomfanya ajiamini kiasi hicho. Pili, kila muujiza alioonesha Musa ulitofuatiana kabisa na uchawi, Miujiza yote ilidhihirisha nguvu isiyo ya kawaida kwa sababu uchawi hauwezi kugeuza fimbo kuwa nyoka halisi. Ndio maana Firauni na washirika wake wakasema kuwa

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 10

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 10

....Musa ni "mchawi" mkubwa (40:24), (7:109). Jina "mchawi mkubwa" kama ilivyokwishaeleza lilificha ukweli kwa sababu za kisiasa. Na tatu, ule uzungumzaji wa Musa uliojaa hekima na hoja zinazoingia akilini nao pia ulidhirihisha ukweli wa maneno ya Musa kuwa yeye ni Mtume. Firauni alikuwa anamjua Musa vizuri sana kwa sababu aliishi nyumbani kwake. Kwa hiyo aliweza kugundua kuwa Musa hakuwa na uwezo wa kuzungumza hivyo kabla ya hapo. 

Baada ya Musa kuitia msukosuko serikali ya Firauni, mtawala huyo akataka ushauri kwa washirika wake (26:35). Wakamshauri kuwa akabiliane na Mussa kwa nguvu za uchawi. Hivyo, wakamtaka atume watu wapigao mbiu ya mgambo wakusanye wachawi wote wakubwa yaani 'magwiji' ili kumkabili Musa (26:36-37). Ikumbukwe kuwa kulikuwa na mamia ya wachawi katika nchi hiyo ambao mara nyingi walikuwa wakifanya mazingaombwe kwa lengo la kujipatia zawadi na tuzo. Kwa maneno mengine uchawi, kwa watu hao ulikuwa kama ajira. Ndio maana walipoitwa kwa Firauni wakauliza kuwa wangepata ujira gani kama wangemshinda Musa. (7:113). 

Kama ilivyodokezwa awali kuwa, Firauni alikwishaiona hatari ya 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 11

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 11

.....Musa kisiasa kwamba miujiza ya Musa ingewateka sio tu watu wake wa karibu bali hata wananchi wa kawaida pia. Ndio sababu akakwepa kuita miujiza na badala yake akaiita uchawi na akamwita Musa mchawi stadi (26:34). Kauli hizo zililenga kuwapotosha watu ili waone kuwa mbona hata watu wengine wanaweza kufanya uchawi. Kwa hiyo Musa aonekane mchawi tu kama wachawi wengine. 

Mbali na propaganda hiyo, Firauni alieneza propaganda kwa wananchi kuwa Musa amewakejeli wazee wao wa zamani kuwa walikuwa wapotevu na walistahili kuangamizwa. Hivyo wajihadhari naye, sio Mtume bali ni mchawi anayetaka kutumia uchawi wake kukutoeni nchini mwenu. Anataka wana wa Israeili wanyakue tena madaraka kama ilivyokuwa wakati wa Yusuf. Sasa lengo la Firauni na washirika wake lilikuwa ni kuwakusanya wananchi wote nchini ili waone ule uwezo wa wachawi wakubwa ambao alitaraji ungevuruga shabaha ya Musa. Firauni aliamini kuwa mara wale wachawi watakapoyazuga macho ya watazamaji yaone fimbo zao kuwa ni nyoka, athari za muujiza wa Musa zingefutika vichwani mwa watu. 

Ni kwa sababu hiyo, walikubaliana na Musa kuwa mpambano huo ufanyike siku ya sikukuu ili 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 12

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 12

....watu kutoka sehemu mbalimbali washuhudie.

Na ufanyike mahala pa wazi, asubuhi kweupe ili watazamaji waone vizuri. Kutokana na uzito na umuhimu wa pambano hilo, Firauni alitoa ahadi nono kwa wachawi wake kwamba wangepata cheo cha kuwa karibu naye (7:114).

Firauni na washirika wake wakaliona pambano hilo kama karata yao muhimu ya kumshinda Musa ili kunusuru madaraka yao, hivyo watu wakahamasishwa mno kuhudhuria pambano hilo.

Walitangaziwa propaganda kuwa Musa "anataka kuwatoa katika nchi yao" (20:57). Pili "anataka kuvuruga mfumo wao wa maisha na kuleta matata katika nchi". (40:26). Tatu mchawi anayetaka kundoa sera zao zilizokuwa bora kabisa (20:63). 

Kwa hiyo basi, nusura ya dini yao na nchi yao ilitegemea nguvu za wachawi wao. Yaani nchi yao pamoja na utaratibu wao wa maisha vitasalimika iwapo tu upande wao utashinda. Hiyo ni kusema kuwa kama Musa akishinda na watawala kupoteza madaraka yao ndio basi tena mfumo wa maisha utabadilishwa na kwa ajili hiyo, utamaduni wao, sanaa zao, ustaarabu wao na vizazi vyao vyote vitaangamia. 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 13

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 13

....Kwa ujumla propaganda zote hizo zililenga kuwashawishi watu waiunge mkono serikali katika mapano ayo.

Majibizano baina ya Musa na Firauni, tena baina ya Musa a.s. na wachawi, na hali ya Musa ya kuogopa kushindwa mbele ya wachawi, na fimbo yake ilipo zimeza kamba zao, na tena mwisho vipi yalivyo ishia mambo ya wachawi na kuamini kwao, na Firauni kuwaadhibu. Kisha ikatajwa vipi Musa alivyo  toka yeye na Wana wa Israili kutokana na Firauni,musa alikimbia na wana wa islaer mpaka wakafika pwani ya bahari wana wa israeli awaoni njia nyingine wamwambia musa kwani umetuleta uku wakati akuna njia?

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 14

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 14

....musa akawambia tamkeni maneno ya kisha akawafundisha dua, au fimbo yake kuichapa kwenya maji bahari ilipasuka katikati na ikahacha njia musa na watu wake wakavuka na vipi alivyo zama Firauni, naye alikuwa kawafuatia baada ya kupasuka bahari kufika katikati bahari   ikarejea ali yake yake ya kawaida na firauni akawa mwenye kuangamia.

vipi Musa aliokoka akafika Jabal T'ur akawaacha watu wake ili ende kwenye mlima kuzungumza na Mola wake Mlezi.

Watu wake walilia njaa nakisha musa akaomba kwa mola mlezi chukula kutoka peponi na chakula kipatikan

Na Msamaria akawafitini kwa kuwachochea waliabudu sanamu la ndama lililo undwa kwa dhahabu. Na ilikuwa ukipita upepo ndani yake hutoa sauti. Musa alikasirika kwayaliyo tokea, akamkamata kichwa nduguye akimvutia kwake. 
Kisha katika Sura hii tukufu  yakatokea yaliyo msibu Msamaria. Mwenyezi Mungu Subhanahu amesimulia hadithi ya kuvuka katika hadithi za Musa nanyinginezo. Na mwisho wa Sura pana mausio mema juu ya Subira, na Usamehevu, na Sala. Kisha ikabainishwa kubwatika washirikina katika matakwayao ya muujiza mwengine usio huu wa Qur'ani; na Subhanahu ameashiria hikima ya kuwatuma Mitume. Tena Sura hii tukufu imekhitimisha kwa kuashiria adhabu watakayo pata makafiri, na malipo mema watakayo pata Waumini. 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 15

      KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 15

Kuna wakati nabii Musa (‘Alayhi Ssalaam) alimuuliza Allah (Sub-haanahu wa-ta’aala): “Ewe Allah, Umenitunuku heshima maalum ya kuongea Nawe moja kwa moja. Je, kuna yeyote mwingine uliyempa heshima hii?” Allah Alimjibu: “Ewe Musa, katika zama za mwisho kutakuwa na umma, nao utakuwa ni umma wa Muhammad (Swalla-llahu ‘alayhi wasallam) watakaokuwa na midomo na ndimi zilizokauka, miili iliyodhoofu, macho yaliyozama, maini makavu, na matumbo yenye njaa --- wao wataniita (ktk du’a zao) Nami nitakuwa karibu yao mno kuliko Nilivyo kwako. Ewe Musa, unavyoongea nami, kuna vizuizi 70,000 baina yako na Yangu, lkn hakutakuwa na kizuizi baina Yangu na umma wa Muhammad (SAW) wakati wanapofuturu. Ewe Musa, Nimejitwisha dhamana kuwa Sitaikataa du’a ya mwenye kufunga wakati wa anapofuturu!”
Sub-haanallah! Ndugu zangu, tuitumie fursa hii ya kumuomba Allah, wkt wa kufuturu, yale tunayoyahitaji!

Basi katika  awo wana waisrael baada ya kuvuka salama kwa bahari kupasuka na kupata chakula kutoka peponi
Miongoni mwao walimsifu musa na kumuliza musa katika dunia hii kuna mtu ana elimu zaidi yako?

Musa alidai kuwa na elimu kubwa zaidi ya mtu yoyote duniani.

Mwenyezi Mungu akamsahihisha kwa kumwambia kuwa amtafute hidhri ili kuipima elimu yake.

Musa akaambiwa aende na samani aliyeokwa, na mara atakapoona samaki huyo katoweka, basi hapo ndipo atakapomuona hidhri.
Musa akatoka na mtu wa kuandamana naye, na walipofika sehemu fulani, samaki huyo aliyeokwa akapata uhai na kutorokea majini. Ni mahali hapa ambapo Musa na mtu aliyeandamana naye wakakutana na hidhri.
Katika Qur’an, kiumbe huyu ametajwa kama mja mchaMungu aliyekuwa na ilimu nyingi kutoka moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu. “Basi wakamkuta mja katika waja wetu Tuliyempa Rehema kutoka Kwetu, na tuliyemuelimisha ilimu (nyingi) zinazotoka Kwetu.” (18:65)

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 16

    KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 16

Hidhiri ni nani?

Hidhri ni kiumbe wa kutatanisha aliyetajwa katika Sura ya 18 ya Qur’an (Surat al-Kahf), aya ya 62 hadi ya 82. Ni kiumbe aliyefanya mambo ya ajabu nje ya Elimu aliyokuwa nayo Nabii Musa aliyepata fursa ya kuongozana naye.
Katika Kitabu chake, The History of al-Tabari, Mwanazuoni na Mwanahistoria wa Kipersia na mfasiri wa Qur’an, Muhammad ibn Jarir al-Tabari ameandika kuhusu Hidhri katika sura iitwayo, “Kisa cha Hidhri na Historia yake, na Historia ya Musa na Mtumishi wake, Joshua.”
Katika maudhui ya Kitabu hicho, Al-Tabari anatoa maelezo ya hadithi ya kale inayomuhusu Hidhri. Mwanzoni mwa Sura hiyo, al-Tabari anafafanua kuwa -Hidhri aliaminika kuwa ni mtoto wa mtu mmoja aliyemwamini Ibrahim au mfuasi wa Ibrahim ambaye aliondoka pamoja na Ibrahim pale alipohama Babylon.
Aidha Hidhri anaaminika kuwa alikuwa na mamlaka katika himaya ya Mfalme Dhul-Qarnaiyn ambaye katika Kitabu hiki anatambuliwa kama Mfalme Afridun.
Hivyo, hidhri ni mtu aliyeishi kabla ya enzi za Nabii 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 17


KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 17

Musa. Katika kitabu hicho, hidhri anatajwa kukutana na Mto wa Maji ya Uzima au maji ya uhai.
Akiwa hajui vilivyomo ndani ya mto huo, akanywa maji yake, na, hivyo, kuwa mtu mwenye uhai mrefu. Ina maana kuwa uhai wake mrefu umetokana na maji ya uhai aliyokunywa bila yeye mwenyewe kujua.

Kuba ya Hidhri, Hekalu la Mji mkongwe wa Jerusalem
Pia hidhri amekuwa akifananishwa na Elijah, lakini Al-Tabari anamtofautisha na Elijah kwa kusema kuwa ahidhri ni Mpesia na Elijah ni Muisraili.

Al-Tabari anaelekea zaidi kuamini kuwa Hidhri aliishi katika kipindi cha Afridun (Dhul-Qarnain) kabla ya Musa kuliko kuamini kuwa aliandamana na Ibrahim, na kuliko kuamini kwamba alikunywa maji ya Uzima (Water of Life).
Al-Tabari haelezi wazi kwa nini amependelea kuamini hivyo, bali anaonekana kuipendelea isinadi ya kisa cha kwanza (cha enzi za Afridun-Dhul-Qarnain) kuliko kisa cha pili.
Maelezo mbalimbali ya Kitabu cha al-Tabari ama yanalingana zaidi au kidogo na maelezo ya Qur’an.

Katika simulizi mbalimbali za Waislamu na wasiokuwa Waislamu, hidhri ameelezewa kama Nabii au 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 18


KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 18

Ni kisa cha  hidhri ameelezewa kama Nabii au Walii au hata Malaika aliye ahi mpaka leo hii ni nabii ambaye bila ya musa uwenda tusinge mfaham

....Walii au hata Malaika. Nchini India, hidhri amefananishwa na Vishnu.

Nchini Iran, amefananishwa na Sorush, Nchini Amenia, amefananishwa na Mtakatifu Sarkis, “the Warrior” na amefananishwa na Yohana Mbatizaji. Na kule Asia Minor, amefananishwa na Mtakatifu George, na kadhalika.

Katika sherehe yake ya tafsiri ya Qur’an, Tafhimul-Qur’an, The Meaning of the Qur’an, Mfasiri Sayyid Abul ‘Ala Maududi yeye kasema kuwa yumkini Hidhri alikuwa ni Malaika kwa sababu ya mambo ya ghaibu aliyoyafanya.

Anasema, katika Sheria na kanuni za kibinadamu huwezi kumuhukumu mtu kabla hajatenda dhambi kama alivyofanya Hidhri kwa yule kijana aliyemuua kwa sababu atakuja kuwaaharibu wazazi wake.

Tangu hapo, mwanadamu wa kawaida asingeweza kujua maisha ya baadae ya mtoto huyo. Huu ni mtazamo wa Maududi.

Kilugha, kwa sababu ya kufanana kilugha kati ya jina hidhri na jina al-akhdar la Kiarabu lenye maana ya kijani, maana ya jina hidhri, mara nyingi, hasa katika lugha ya mazungumzo, na hata kitaaluma, huwa ni “Mtu wa Kijani”.

Baadhi ya Maulamaa wanaikataa maana hiyo. Hata hivyo, Maulamaa wengine wanaonesha uwezekano wa kumfananisha na mtu mmoja wa Mesopotamia, Utnapishtum. Kwa mujibu wa mtazamo mpya, Hidhri si 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 19

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 19

....neno la Kiarabu.

Katika Jamii ya Waislamu wa Suni, ingawaje Wanazuoni wa Sunni wanakhitilafiana rai juu ya iwapo hidhri bado yuhai, lakini miongoni mwa Masufi wa Kisunni, kuna maafikiano kuwa hidhri bado yuhai huku watu wa kuheshimika, na Masheikh, na Maimamu wakubwa wakidai kuwa wamekutana ana kwa ana na mja huyu, hidhri.

Mifano ya watu waliosema wamekutana na hidhri ni Sheikh Abdul Qadir Jaylani, Sheikh al-Nawawi, Ibn Arabi, Sidi Abdul Aziz ad-Dabbagh na Ahmad ibn Idris al-Fasi.
Kwa mujibu wa Lata’if al-Minan (1:84-98), kuna maafikiano miongoni mwa Masufi kuwa hidhri bado yuko hai.
Katika duru za Twariqa, watu wa Twariqa, Zawiyyah, Idrisiyya, Muridi, wanampa al-Khidhri nafasi adhimu katika maono yao ya ndani na mawanda yao ya kiroho. Katika jamii ya Masufi, al-Khidhri ni mtu yoyote anayepata nuru inayotoka moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu bila taamuli ya kibinadamu.
Kwa mujibu wa Sufi mmoja wa Sri Lanka, Bawa Muhaiyaddiin, hidhri alikuwa ni mja aliyefanya jitihada za muda mrefu za kumtafuta Mungu hadi Mwenyezi Mungu, kwa rehema Zake, akamtuma

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 20

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 20

....Jibril kwenda kumuongoza.
Jibril akajitokeza kwa hidhri kama mwalimu wa kibinadamu mwenye hekima, na hidhri akampokea Jibril kama mwalimu wake. Jibril akamfundisha hidhri vilevile kama hidhri alivyokuja kumfundisha Musa baadae kwa kufanya matendo ambayo yalionekana kama ni ya kidhalimu.
hidhri akavunja mara kwa mara ahadi ya kutosema jambo la kupinga matendo ya Jibril, na bado hakuwa amejua kwamba mwalimu yule wa kibinadamu alikuwa ni Jibril.

Kisha Jibril akafafanua matendo aliyoyafanya, na akabainisha umalaika wake kwa hidhri. Ndipo hidhri alipotambua kuwa kumbe Mwalimu yule alikuwa ni Malaika Jibril aliyemjia kwa sura ya kibinadamu.

Katika Sura ya 18, aya ya 65-82, Musa anakutana na mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu ambaye Mwenyezi Mungu anasema, “Tuliyempa Rehema kutoka Kwetu, na tuliyemuilimisha ilimu (nyingi) zinazotoka Kwetu.”

Maulamaa wa Kiislamu wanamtambua kama hidhri ingawaje hatajwi waziwazi katika Qur’an, na hakuna utajo wa wasifu wake wa kimaumbile. Qur’an inaeleza kuwa Musa na hidhri walikutana kwenye makutano ya bahari mbili.

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 21


KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 21

.....Kukutana kwao kulitanguliwa na tukio la ajabu la samaki wa chakula cha safari cha Musa na Kijana wake kutorokea baharini. “Na walipofika mbele, (Musa) akamwambia kijana wake, “Tupe chakula chetu cha asubuhi; maana tumepata uchovu katika safari yetu hii.

(Kijana wake) akasema, “unaona basi! Pale tulipopumzika katika mlima, nimesahau kukupa habari ya yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha isipokuwa Shetani, nisikumbuke. Naye (samaki) akashika njia yake baharini kwa namna ya ajabu.

(Musa) akasema: ‘Hapo ndipo tulipokuwa tunapataka.’ Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia yao (ileile). Basi wakamkuta mja katika waja Wetu….”

Baada ya kukutana, Musa akaomba ruhusa ya kuongozana na Mja huyu wa Mwenyezi Mungu ili aweze kujifunza kwake ‘ilimu sahihi ya yale ambayo amefundishwa.

Mja huyo akamwambia Musa kwa uzito kuwa asingeliweza kuvumilia kuandamana naye kwani asingeliweza kuyavumilia mambo asiyoyajua undani wake.
Musa akasema nitakuwa na subira wala sita kuasi

Musa akaahidi kuwa angekuwa mvumilivu inshaAllah. 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 22


KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 22

....Mja huyo akatahadharisha kuwa kama wangeongozana basi asingependa Musa amuulize-ulize kuhusu yale ambayo angeyaona mpaka nitakapo kuja kukuhadisia

Musa akaahidi kuwa angekuwa mvumilivu inshaAllah.

Basi wakondoka kuanza safari wakafika bwani ya bahari wakakuta majazi mengi
Wakomba wasika wapande jaazi kwakua walikuwa awana nauli wakalusiwa

walipopanda jahazi safari ikaanza walipofika katika ya bahari bahari ikachafuka, hidhri akatoboa jahazi hilo maji yakaingia jaazini. Musa akakiuka ahadi yake kwa kushindwa kulivumilia jambo hilo. Akauliza, mbona tena unatoboa jahazi, unataka kuzamisha watu ? Hakika umefanya jambo baya.

Mja huyo akamkumbusha Musa kuhusu ile tahadhari aliyompa. Sikukwambia kwamba huwezi kuvumilia kuongozana nami kisha ukafanya subira?  

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 23

        KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 23

...Musa akaomba samahani kwa kusahan nakusema ilikuwa mara yake ya kwanza.

Baada ya tukio hilo, Mja huyo akafanya tukio jingine la kumuua kijana mmoja. Kwa mshangao na masikitiko, Musa akalalamika na kusema umefanya jambo baya kabisa umeua nafusi ya mtoto asiyekua hatia?

Hidhri akakumbushia tena ile tahadhari yake kua awezi kufanya subra. Musa akaahidi kuwa hatovunja tena ahadi yake sitokuliza tena nikikuliza tena basi unifukuze nisiongozane na wewe tena katika safari yako idhili akamsamee musa

Wakaendelea na safari yao hadi wakafika katika mji ambao wenyeji wake walishindwa kuwakirimu walinyimwa chakula na malazi mpaka walipie basi wakanunua kila walichoitaji kisha wakaendela na safiri walipofika mbele kidogo yakijiji icho wakakuta ukuta umedondoka 

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 24


KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 24

....Na watu wa mji ule wanajaribu kuinua umeshindikana licha ya hivyo, hidhiri akainua ukuta uliobomoka kwa mikono yake ukuta ukasimama katika mji huo.

Kwa mara nyingine, Musa akamuona hidhri kama mtu wa ajabu, na akavunja ahadi ya uvumilivu kwa mara ya tatu, akihoji, kwa nini asiwatoze watu wa mji huo malipo ya kazi hiyo?

Mja huyo akamwambia Musa, hapa ndipo tunapofarakiana mimi na wewe. Ngoja sasa nikufahamishe undani wa mambo ambayo wewe hukuweza kuyavumilia.

Kuhusu Jahazi, akamwambia liliharibiwa ili kuwakinga wamiliki wake wasiangukie mikononi mwa mfalme aliye kuwa jodani ambaye alikuwa akikamata kila jahazi nzuri kwa nguvu ila ikiwa na dosari uiwiacha ndio mahana mimi nimeitoboa ili isichukuliwe. Tukio hili ni ishara kuwa kumbe jambo linaloweza kuonekana baya na la shari huweza kuwa na kheri na matokeo mazuri kabisa.

Na kuhusu kijana yule, wazazi wake walikuwa waumini, na ilihofiwa kuwa asije akasababisha wazazi wake waasi na kukufuru.Mwenyezi Mungu angewajaalia mtoto mwingine mwema ambaye angepambika kwa utakaso nakweli mola aliwajiria mtoto wa kike ndio alikuja kuwa mama mzazi wa yunus bin mataa.

ITAENDELEA......

                IN SHAA ALLAH

                      SEHEMU YA 25

KISA CHA MUSA NA HIDHIRI

                   SEHEMU YA 25

....Na kuhusu Ukuta ulioinuliwa, chini ya ukuta huo kulikuwa na hazina ya mayatima ambao baba yao alikuwa mcha Mungu. Akiwa kama mjumbe aliyetumwa na Mwenyezi Mungu, Al-Hidhri akauinua ukuta huo, hapa Mwenyezi Mungu akiulipa wema wa baba mchaMungu wa mayatima hao ili mayatima hao wakikua waione na kuitumia hazina yao.mambo ayo sikuyafanya kwa amri yangu isipokuwa kwa elimu ya aliyonipa ALLAH.

hidhri alivyoelezewa katika Hadiyth

Miongoni mwa dalili kuhusu maisha ya hidhri ni riwaya mbili; moja iliyosimuliwa na Imam Ahmad ibn Hanbal, katika Al-Zuhd ambapo Mtume ameripotiwa kusema kuwa Elijah na hidhri hukutana kila mwaka katika Mwezi wa Ramadhani mjini Jerusalem.

Na riwaya nyingine ilisimuliwa na Ya’qub ibn Sufyan kutoka kwa Umar kwamba mtu aliyeonekana kuongozana naye alikuwa ni hidhri. Ibn Hajar akabainisha kisa cha kwanza na cha pili kuwa vyote ni sahihi. Taz. Fath al-Bari (1959 ed. 6:435).

Akaendelea kutaja riwaya nyingine sahihi iliyosimuliwa na Ibn Asakir kutoka kwa Abu Zur’a al-Razi ambapo Abu Zur’a al-Razi alikutana na hidhri mara mbili; ya kwanza wakati wa ujana wake, na ya pili wakati wa uzee wake, lakini hidhri mwenyewe alikuwa hakubadilika haiba.

Hidhri anaaminika kuwa na haiba ya kijana na mtu mzima, mwenye ndevu ndefu nyeupe. Kwa mujibu wa waandishi kama Abdul Haq Vidhyarthi, Hidhri ndiye Xerxes (asichanganywe na Xerxes I) ambaye alitoweka baada ya kuingia katika mikoa ya kanda ya Ziwa ya Sistan.

Mikoa hiyo inajumuisha nchi za majimaji za mpakani mwa Iran na Afghanistan hivi leo, na baada ya kupata eneo la kuishi, akaazimia kuishi maisha yake yote yaliyosalia akimtumikia Mungu na kuwasaidia wale waliopita katika njia ya kumfuata Mungu.
Muhammad al-Bukhari kasimulia kuwa hidhri alipata jina hili baada ya kujitokeza juu ya uso wa ardhi ambao uligeuka rangi ya kijani baada ya yeye kujitokeza hapo.
Kuna riwaya kutoka kwa Bayhaqi kwamba hidhri alihudhuria mazishi ya Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam, na alitambuliwa na Swahaba Ali miongoni mwa Maswahaba waliokuwepo.
Hidhri alikuja kuonesha huzuni na majonzi yake juu ya kifo cha Mtume Muhammad. Tukio la hidhri kuhudhuria mazishi ya Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam, linaelezwa hivi:
Mtu aliyeonekana kuwa na nguvu, haiba nzuri na mtanashati mwenye ndevu ndefu nyeupe alijitokeza akiwaruka mgongoni watu (waliokaa) hadi akafika pale ulipolazwa mwili wa Mtume Muhammad. Huku akilia kwa uchungu, aliwageukia Maswahaba na kuomboleza. Ali ibn Abi Talib akasema, mtu huyo alikuwa ni hidhri.
Katika simulizi nyingine, hidhri alikutana na swahaba mmoja katika eneo la Ka’aba na akamfundisha swahaba huyo dua ambayo ni yenye thawabu sana pale inaposomwa baada ya Swala za Faradhi. Hii imesimuliwa na Imam Muslim.

Nainasemekana hidhiri upendelea kujitokeza kwenye misikiti mbali mbali asah katika swala za subhui na al asiri
Ndio mahana tunapendelea kupeana mikona baada ya swala na hii inasemekana ukikuta mkono laini sana kama akuna mfupa basi uwenda uyo ni hidhiri.
Jambo ilo ulipatapo mwambie akuombee dua.

                        MWISHO

KISA ICHI KIMEKUSANYWA NA KUANDALIWA VEMA NA TAWFIQ  MASSINI
Simu nam 0784 699901