SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 12 Aprili 2018

T media news

CAG Aionya Serikali Kuhusu Mikopo

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad ameitahadharisha serikali kuhusu kukopa na kusema kuwa wanapaswa kuwa makini ili kuendelea kupunguza gross late zaidi kwa siku za mbele.

Prof. Assad amesema hayo leo April 11, 2018 mjini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu.

"Si busara sana kutazama eneo hilo na kusema basi tunaweza kukopa kwa sababu si busara kwani tuliwahi kukopa tukapunguziwa mikopo yetu kwa hiyo mimi rai yangu ni kwamba lazima tuwe waangalifu katika ukopaji wetu, mwaka jana tulikuwa na gross late ya asilimia 25 mwaka huu imerudi mpaka asilimia 12 kwa hiyo tumepunguza gross late imepungua kwa hiyo ni muhimu hii gross late ikapungua zaidi tunapokwenda mbele" alisema CAG

Aidha Prof. Mussa Assad, amesema kiasi cha shilingi trilioni 4.58 hakikujumuishwa katika deni la taifa kutokana na kutojumuishwa kwa madeni ya mifuko ya pensheni pamoja na dhamana ambazo masharti yake yalikiukwa.

Mbali na hilo amesema ukaguzi umebaini mapungufu kadhaa yanayohusu fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo na matumizi ya kawaida pamoja na zinazokusanywa kupitia vyanzo ndani vya mamlaka za serikali za mitaa.