SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Machi 2018

T media news

Rais wa Myanmar Htin Kyaw Ajiuzulu

Rais wa Myanmar Htin Kyaw amejiuzulu, kulingana na afisi yake.

Hakuna sababu ilitolewa lakini kumekuwa na wasiwasi katika miezi ya hivi karibuni kuhusu afya ya rais huyo mwenye umri wa miaka 71 baada ya kuonekana amedhoofika katika hafla moja.

Htin Kyaw alliapishwa kuwa rais 2016 baada ya uchaguzi uliositisha miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.

Lakini alikuwa kiongozi asiye na mamlaka huku aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Aung San Suu Kyi akiwa kiongozi mwenye mamlaka.

taarifa iliochapishwa katika mtandao wa facebook wa rais huyo ilisema kuwa Htin alitaka kupumzika.

Makamu wa rais Myint Swe , jenerali wa zamani atakuwa kaimu rais hadi pale rais mpya atakapochaguliwa katika muda wa siku saba sijazo, taarifa hiyo ilisema.