SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 23 Februari 2018

T media news

Wadada: Mtunusuru na Hizi Picha zenu Huko Mitandaoni

Juzi kati nilikutana na mrembo huko facebook. Kupitia picha alizoweka "nikashawishika" na "kuhamasika" kutoa mwaliko pasipo shuruti. Alionekana ni demu aliyekidhi vigezo vyangu alikuwa kimodo fulani hivi maji ya kunde fulani iliyofifia. Mwenyewe nikasema yes.

Baada ya chats za siku kadhaa tukakubaliana kukutana kwenye moja ya maeneo nayoamini sana hasa nikizingatia "ukisu" wa yule demu sikutaka sehemu ya maskharamaskhara. Huku na huko siku na muda vikawadia, demu akanishtua ameshakuja maeneo tuliyokubaliana.

Nami uzuri sikuwa mbali na hapo. Nikajisogeza kidogo nikapishana na dada mmoja kibonge kavaa mlegezo wa jinzi, shati la mikono mirefu lenye rangi ya ugoro huku likiwa limejaa alama za misalaba. Nikampita huyo dada huku nikielekea mashariki huku nikiitafuta ile sura ya fesibuku kulia na kushoto kwa eneo ile bila mafanikio. Punde simu yangu ikaita kucheki dem anapiga.

Akanambia keshaingia amekaa ananingoja, akanielekeza. Nilishangaa kidogo kwa sababu kwa jografia ya pale asingeweza kupita bila kuniona na watu hawakuwa wengi kivile. Kwa Haraka sana machale yakanicheza nikajiuliza asijekuwa ni yule demu wa misalaba niliyepishana naye hapa hivi punde. Maana nilijua kama ni yeye ishakuwa baala hii.

Nikajishawishi kimoyomoyo haiwezekan akawa ni yeye. Njkajitokeza kwenda kumcheki nakuta kumbe ndio dem yuleyule niliepishana nae, tena sasa kashazungukwa na wahudmu wanamsikiza anaagiza mapochopocho. Nikajisemea kimoyomoyo laahaula lakwata.. leo imekula kwangu vibaya. Nilitaka kupiga u-turn kisha nizimishe simu mazima nikaona itakuwa soo zaidi na hata hivo ningemtia hasara.

Nikaamua kuwa muungwana, basi kwa taaabu nikajivuta huku nikilazimisha 'kuitafuta' tabasamu ili demu asijekunishtukia. Tulipiga stori 2-3 nikajifanya kupokea visimu vya uongouongo hapo ili mradi nitafute sababu nitokomee zangu fasta maana hili disko limeshaingiliwa na mmasai.