SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 22 Februari 2018

T media news

Asalam alaykum. Naomba ufafanuzi hivi mtoto mchanga anaponyolewa nywele kwa mara ya kwanza nakisha nywele zake kupimwa na kutolewa sadaka fedha ama dhahabu kwa uzito unaolingana. Jambo hili limethibiti katika dini ama la?

JIBU.

BISMILLAH.

Naam limethibiti, kwa kauli na vitendo, kama tutavyo ona baadae.

Kwanza, AQIIQA ni nini?

Aqiiqa, kwa upande wa lugha, ni nyewele za mtoto mchanga aliyezaliwa nazo.

Kwa upande wa Sharia, Aqiiqa maana yake mnyama anayechinjwa kwa kuzaliwa mtoto, na kunyolewa nywele zake (aqiiqa yake).

Mtume صلى الله عليه وسلم amesema:

كل مولود مرهون بعقيقته تذبح عنه يوم سابعه ويحلق ويسمى (رواو أبو داؤد (2838) أحمد (5.7) النسائى(4220) Kila mtoto aliyezaliwa yumo kwenye rehani mpaka achinjiwe mbuzi wake siku ya asaba, na anyolewe nywele, na kupewa jina”  Abu DAud, Ahmad na Nasai.

Hivyo, Aqiiqa ni Sunna kukbwa sana, (isipokuwa kwa Abu Hanifa, yeye anasema Si sunna wala Si faradhi, ni jambo la kujitolea tu)

Kwa upande wa maulamaa wengine, hata hivyo, Aqiiqa ni Sunna iliyotiliwa mkazo, سنة مؤكدة  sawa sawa na Mbuzi wa Udh-hiya, kwa upande wa masharti yake, aina ya mnayma, na umri wa mnyama huyo.

Miongoni mwa masharti yake ni kwamba asiwe na kilema chochote, na asiwe chini ya umri wa miaka mwili. Na ni kondoo au mbuzi. Ila inajuzu, vile vile, kwa mwenye uwezo zaidi, ngamia au ng’ombe. Yaani, ngamia bora kuliko ng’ombe, na ng’ombe bora kuliko mbuzi au kuondoo.

Sunna ya Aqiiqa kwa mtoto wa kiume ni mbuzi wawili na kwa mtoto wa kike mbuzi mmoja.

Na mwenye jukumu al kuchinga na Mzee wa mtoto: Baba kwanza, anafuatiwa na Babu, Ami, Kaka mkubwa na kadhalika.

Wakikosekana wanaumbe basi upande wa kuukeni: Mama mzazi, Bibi, Shangazi, Khaloo (mama mdogo), Dada na kadhlika.

Na gharama za mnyama zitoke kwenye mali ya Mzazi, na SI kutoka kwenye mali ya mtoto mwenyewe aliyezaliwa (iwapo kuna urithi wake).

KUCHINJA SIKU YA SABA NA KUPEWA JINA

Aqiqa inatakikana achinjwe Siku ay Saba, baada ya kuzaliwa mtoto, na mtoto anyolewe nyewele, kwa mara ya kwanza, na kisha zipimwe kwa madini kama fedha, na uzito wa madini hiyo utolewe sadaka.

Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume صلى الله عليه وسلم kwa wajukuu zake wawili, al-Hasan na al-Husayn. Aliwachinjia wanyama kondoo wawili,  wa mkono wake mtukufu.

Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنه  akisema: Aliwachinjia Aqiiqa Mtume صلى الله عليه وسلم al-Hasan na al-Husayn kondoo kila mmoja” Abu Daud H.2841.

Na imepokewa kutoka kwa Ibn Abbs رضي الله عنهما akisema: Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Aqiqa ya msichana ni mbuzi mmoja na aqiiqa ya mvulana ni mbuzi wawili” Abu Daud.

Vile vile imepokewa kutoka kwa Umm Kurz al-K’abiyya رضي الله عنها akisema: Nimesika Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: Aqiiqa ya mvulana ni mbuzi wawili wanaofanana (umri na sifa) na ya msichana ni mbuzi mmoja” Abu Daud, Kitaab al-Adhaahi, H. 2834.

KUPEWA JINA SIKU YA SABA

Na siku hiyo hiyo, BAADA YA KUCHINJWA AQIIQA, anapewa jina mtoto, iwapo bado hajapewa.

Ama ikiwa ameshapewa jina, mara tu baada ya kuzalia, au aliekewa jina hata kabla ya kuzaliwa, na akapwa mara tu baada ya kukzaliwa, basi siku hiyo ya Saba itakuwa ni SIKU ya kulithibitishwa rasmi jina hilo, baada ya kuchinjiwa Aqiiqa yake.

Bora ya majina ni lile lenye kuambatanishwa na Allah, au mojawapo wa Majina Yake Matakatifu, kama Abdullah, Abdufattah, Abdulqadir, Abdulwahaab, Abdulghafuur na kadhalika, kwa mtoto wa kiume.

Kwa upande wa watoto wa kike, basi bora majina ya waja wema waliotangulia, Maryam, Aasiya, Fatma, Khadija, Zaynab, na kadhalika.

Na hakuna ukaraha wala junaha kumpa majina ya ukoo, au kumbukumbu ya mmojawapo wa wazazi wake, na kadhalika. Ilimradi yasiwe majina mabaya, kama Mwanashari, Magomvi, Punda, Zuzu, Zumbukuku na kadhalika; Mtumeصلى  الله عليه وسلم  ameusia kuwapa watoto majina mema, na SI majina ya kuashiria uovu au ubaya.

Na ni haramu kumwita kwa majina ya Mwenyezi Mungu; kama al-Ghafuur, lakini Ghafuur inajuzu, al-Shakuur haramu, lakini Shakuur inajuzu. Al-Aziz haramu, lakini Aziz inajuzu, na kadhalika.

MUDA WA AQIIQA.

Muda wa Aqiqa ni tanagu kuzliwa mtoto hadi kubalighi. Lakini akishabalighi basi fadhila za kufuata Sunna hazipo tena. Ila thawabu za Sadaka zipo pale pale.

Hata hivyo, yule ambaye anaamini kuwa hajachinjiwa Aqiiqa na wazee wake, basi anaweza kujichinjia mweyewe utuuzimani. Kwani – kama tulivyosema- Aqiqa ni Sunna kubwa iliyotiliwa mkazo sana, na ni kama mbuzi wa Udh-hiya.

Na isitoshe, Mtume صلى الله عليه وسلم alijichinjia Aqiiqa baada ya kupewa Utume. Al-Bayhaqi fi al-Sunan al-kubra, Babb al-Aqiiqa Sunna: H. 9/300. Bidaayat al-Mujtahid 1/475.

NYAMA YA AQIIQA.

Nyama ya Aqiiqa inatolewa sadaka kwa masikini, na vile vile kwa wanafamilia. Hivyo inajuzu watu wa nyumbani kula nyama hiyo. Ila ni makuruhu kumlisha chochote aliyechinjiwa Aqiiqa hiyo.

KUNYOLEWA NA KUPIMWA NYWELE ZAKE KWA MADINI.

Kama tulivyosema, mnyama wa Aqiiqa anachinjwa siku ya Saba, tokea kuzaliwa mtoto, na baadae hupewa jina, na baadae hunyolewa na kupimwa nywele zake kwa madini, na uzito huo kutolewa sadaka. Kwa utaratibu huo: SIKU HIYO HIYO.

Ikishindikana siku ya Saba, basi siku ya 14. Ikikosekana siku ya 14, basi sikuu ya 21, na kuendelea hivyo hivyo. Bi. Aisha رضى الله عنها alisema hivyo kuwajibu waliokuwa wakimuuliza swali hilo.

Shafiiyya na Maalikiyya, wanasema Sunna kuchinja, kumpa jina, kumnyoa nywele, kuzipima kwa madini, ama dhahabu au fedha na kutoa sadaka thamani ya madini hiyo.

Hanabila wanasema utaratibu huo huo, ila kwao wao sunna ni madini ya fedha tu.

Abu Hanifa – kama tulivyosema, kwake yeye ni jambo la kujitolea tu-; hivyo itategemea unataka kujitolea nini. Ni sadaka tu. Haina mpango wowote ule.

Dalili ya Shafiiyya, Mlikilyya na Hanabila  ni pamoja na Hadtihi zifuatazo:

ما رواه علي بن أبي طالب قال: عق رسول الله صلى الله عليه وسلم عن الحسن بشاة، وقال: يا فاطمة احلقي رأسه، وتصدقي بزنة شعره فضة، قال: فوزنته فكان وزنه درهماً أو بعض درهم. رواه الترمذي.. وعن أبي رافع قال: لما ولدت فاطمة حسناً قالت: ألا أعق عن ابني بدم؟ قال: لا، ولكن احلقي رأسه وتصدقي بوزن شعره من فضة على المساكين والأوفاض، وكان الأوفاض ناساً من أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم محتاجين في المسجد أو في الصفة. رواه أحمد

Imepokewa na Sayyidina Aliyy bin Abi Twaalib رضي الله عنه akisema: Aliwachinjia Aqiiqa Mtume صلى الله عليه  سلم al-Hasan na al-Husayn mbuzi mmoja kila mmoja, na akamwambia Fatma: “Wanyoe vichwao vyao, na toa sadaka uzito wa fedha wa nyewele zao hizo. Anasema Sayyidina Aliyy: basi nikazipima na uzani wake ukawa sawa na dirham mmoja nakitu hivi” Ameipokea  Tirmidhi.

Na imepokewa kutoka kwa Abu Raafi’ رضي الله عنه akisema: Alipomzaa al-Hasan Bi.Fatma aliuliza kwa kusema: “Je, naweza kumchinjia mtoto wangu mnyama?  Mtume صلى الله عليه وسلم akamjibu: “Hapana! Lakini mnyowe nyewele zake, na zipime kwa fedha, na toa sadaka fedha hiyo ka masikini, na kwa Aqfaadh (na Awafaadh ni mafaqiri wa kibaraza cha Suffa cha kando ya Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وسلم  ). Ameipokea Imam Ahmad.

NB. Mtume صلى الله عليه وسلم si kama alimkataza Bi. Fatma kuchinja aqiqa, bali ni kwamba alitaka kuifanfya Sunna hiyo YEYE Mwenyewe, ndiyo maana akamwambai Wewe wanyoye tu na pima nywele zao kwa fedha na toa sadaka fedha hiyo.  Maana, kama tulivyo ona hapo juu na tutavyo ona katika hadithi zifuatazo, Mtume صلى الله عليه وسلم aliwachinjia al-Hasan na al-Husayn kondoo wawili kwa mikono yake mwenyewe.

HADITHI ZAIDI KUHUSU AQIQA.

1. فعن سَلْمَان بْن عَامِرٍ الضَّبِّيّ قَالَ: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:مع الغلام عقيقة، فأهريقوا عنه دماً، وأميطوا عنه الأذى. رواه البخاري.   Imepokewa na Salmaan bin Aamir al-Dhwabbi رضي الله عنه akisema: Nimemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: Kila mtoto anasahiki kuchinjiwa Aqiqa wake. Hivyo basi, mchinjieni mwage damu kwa kuzaliwa kwake, na muondosheeni maudhi” Bukhari.

2. وعن عائشةَ:أن رسول الله صلى الله عليه وسلم أمرهم عن الغلام شاتان مكافئتان، وعن الجارية شاة. رواه الترمذي وقال حسن صحيح، وابن ماجه،   Imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha رضي الله عنها akisema: Aliwaamrisha Mtume صلى الله عليه وسلم wamchinjie mvulana mbuzi wawili wenye umri sawiya, na msichana mbuzi mmoja”.  Ameipokea Tirhimdi na Ibn Majah. Amesema Tirmidhi ni Hadithi Hasanun Swahih.

3. Imepokewa kutoka kwa Imm Malik, kutoka kwa Jafar bin Muhammd kutoka kwa Muhammad bin Aliyy Zayn al-Aabidiin akisema: وزنت فاطمة بنت رسول الله صلى الله عليه وسلم شعر حسن وحسين وزينب وأم كلثوم فتصدقت بزنة ذلك فضة “Bibi Fatma alipima nywele za al-Hasan, al-husayn, na Zayna, na Ummu Kulthuum, kila mmoja kwa fedha na kutoa sadaka kwa uzito wake” Muwatta

4. Imepokewa kutoka kaw Aliy bin al-Husayn bin Aliyy bin Abi Twalib akisema: Alipima Fatma Binti wa Mtume صلى الله عليه وسلم nywele za Hasan na Husayn kwa fedha na akatoa sadaka uzito wake huo” Muwatta’.

NYONGEZA.

Mila ya kuchinja Mnyama wa Aqiqa ilikuwepo tokea zama za Ujjahiliyya: kama sadaka na kumuondolea mtoto kijicho na hasad. Ila walikuwa na ada ya kumpaka damu ya mnyama huyo, kama ishara ya kuwa ameshafanyiwa Aqiqa.

Uwislamu ulipokuja, haukupiga marfukufu Aqiiqa, kama ilivyokuwa hakupiga marufuku wanyama wa Udh-hiya.  Ila ulipiga marufuku kumpaka mtoto damu ya Aqiiqa, wakiamini kuwa damu hiyo ndiyo unamlinda na kumhami. 

Badala yake ukaachia wazi waislamu kufanya lolote lile ambalo halina ushirikina wala mila za kishirikina. Maswahaba walikuwa na mtindo wa kumpaka mtoto zaafarani, kwenye kipaji; ili kuonesha kuwa ameshafanyiwa Aqiiqa na ameshapewa jina. Hivyo, wale wanaokuja kuwasalimai wazeewa mtoto, wakiona hivyo wanajua kuwa ameshapewa jina. Hizi ni mila ambazo hazina mushkeli. Sisi tulipakwa Hina vipajini, na tumekuwa tukifanya vivyo hivyo kwa watoto wetu na wajukuu zetu.

Imepokewa kutoka kwa Abu Burayda al-Aslamiyy رضي الله عنه  akisema: Zama za Ujahililyya, tulikuwa tukichijja mbuzi tunapopata mtoto wa kiume, na tumapaka kichwa chake kwa damu ya mbuzi huyo. Lakini ulipokuwa Uwislamu, tukawa tunamnyoa nyewele zake na tunampaka zaafarani” Bidayat al-Mujtahidl, 1\476.

KUMUADHINIA MTOTO.

Inapendekezwa, مستحب na waja wema kumuadhinia mtoto sikio lake la kulia na kumqimia sikio lake la kushoto; ili kutabarruk تفاؤلا kwa matumaini mema kuwa Saudi na Qauli ya mwanzo anayo isikia ni Wito wa Swala, na Majina ya Mwenyezi Mungu. Mtume صلى الله عليه وسلم alikuwa haamini kuweko MIKOSI, kila kitu kinatoka kwa Allah, lakini akiamini Fa’l = matumaini mema.  Hivyo, Kumudhinia na kumkimia mtoto mchanga, ikawa miito mwili hiyo ndiyo anayoisikia, mara tu baada ya kuigia katika Dunia hii, ni Fa’l njema. Hakuna mushkeli. 

SUNNA YA KUOMBEWA NA MJA MWEMA.

Sunna nyengine, muhimu, ni kumapta mja mwema, kumuombea dua mtoto mchanga huyo, hata kama kabla ya kutia kinywani chochote kile, na kutafuna kitu kitamu, kama tende, na kisha kuchovya kidole cha mja mwema huyo kwenye mmung’unyo wa tende hiyo, na kumrambisha mtoto mchanga huyo. Hivyo ndiyo alivyokuwa akifanya Mtume صلى الله عليه نسلم pale anapoletewa watoto wachanga awaombee na kuwafungua kinywa.

وبالله التوفيق

الحقير  إلى الله تعالى عبد القادر شريف آل الشيخ