SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 14 Januari 2018

T media news

Matatizombali mbali yanayoweza kujitokeza katika mfumo wa mafuta wa gari lako

Mfumo wa mafuta katika gari umegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni mfumo wa mafuta ya petroli (Petrol fuel system) na mfumo wa mafuta wa Diseli (Diesel fuel system). Katika mada hii tutaangalia tofauti ya aina hizo za mfumo huu pamoja na matatizo yanayoweza kujitokeza katika mfumo huo kwa ujumla.

Tofauti kubwa kati ya mifumo hiyo miwili ni mgandamizo wa kimakanika (mechanical compression), ambapo katika mfumo wa siesel mgandamizo unakuwa mkubwa zaidi kuliko umeme. Tofauti nyingine ni kwamba mfumo wa petroli unatumia ‘spark plug’ kwa ajili ya kuchoma mafuta wakati ule wa diesel unatumia ‘heater plug’ kusaidia injini kuwaka kwa urahisi zaidi.

Nyingine ni katika pigo la kuingizia, ambapo kwenye mfumo wa petroli, hewa na mafuta vinachanganyika pamoja na kuingia katika chumba cha muwako, wakati diesel hewa pekee ndiyo inaingia katika chumba cha muwako.

Matatizo yanayotokea katika mfumo wa mafuta kwa ujumla

Matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwenye mfumo wa mafuta katika gari ni pamoja na , uchafu katika mafuta, kupasuka kwa  mpira wa mafuta, kutofanya kazi kwa pampu, mfumo kuingiwa na maji, mfumo kuingiwa na mafuta tofauti hususani mfumo wa petroli kuingiwa na diesel.

Uchafu katika mafuta

Hili ni iongoni mwa matatizo ambayo yanaukumba mfumo huu kwa ujumla. Uchafu kupita kiasi katika mafuta ni tatizo kwa sababu ufanyaji kazi wa mfumo utaathiriwa kwa kujaza uchafu kwenye chujio, hivyo mafuta husafiri kwa uchache na mwisho kusababisha chombo kisipate moto wa kutosha wa kuwezesha kuwaka inavyotakiwa kutokana na changamoto hiyo (misfiring).

Hivyo ni bora zaidi kutumia mafuta yaliyothibitishwa, lakini pia kufanya matengenezo (service) kwa muda stahiki ili kuepusha gharama kubwa zaidi.

Kupasuka kwa mpira wa mafuta

Tatizo jingine ni kupasuka kwa mpira wa mafuta. Kama inavyofahamika kwamba, gari inatumika katika mazingira tofauti tofauti na pia hukabiliana na mikasa mbalimbali hivyo kuna uwezekano bomba (pipe) ikapasuka au sehemu yoyote katika mfumo kupata hitilafu na kusababisha kuvuja kwa mafuta na hatimaye kuingiza yakiwa pungufu, hivyo kusababisha injini  za chombo kutopokea moto ipasavyo.

Kutofanya kazi kwa  pampu

hili ni tatizo kubwa pia katika mfumo huu, kwani mafuta yasiposukumwa kwa mgandamizo, basi ndipo utendaji kazi wa mfumo unakuwa mzuri zaidi. Iwapo pampu haifanyi kazi kabisa, basi gari haitowaka na kama haifanyi kazi kwa mgandamizo basi gari litawaka lakini injini yake ikiwa haina moto wa kutosha.

Mfumo kuingiwa maji ama mafuta yasiyo sahihi

Kitu kingine ni mfumo ukiingiwa na maji au mafuta tofauti. Kwa mfano mfumo wa petroli kuingiwa na mafuta ya diesel. hili ni tatizo ambalo limewakuta watumiaji na wamiliki wengi wa magari wanapojaza mafuta katika vituo vya mafuta (sheli) mbalimbali na tatizo hili ukilidharau basi utaua na kuharibu vifaa vingi kwenye gari yako na hatimaye kuingia gharama katika utengenezaji na kubadili vifaa zaidi.