Ni ajabu kwamba leo Mbunge Ester Bulaya amekamatwa na anashikiliwa na polisi eti kwa kuja jimboni kwangu kunisaidia kuchangia kwenye ujenzi wa Hostel ya watoto wa kike kwenye shule ya sekondari Nyamongo!!! Mh Bulaya ni Mwanamara, ni Mtanzania na ana haki ya kufanya ushirikiano na mtu yeyote anaetaka,sitakubali kuona viongozi wachache wa serikali wasiokuwa na uadilifu wanahujumu maendeleo makubwa tunayofanya Tarime kisa yanafanywa na chadema, hatutakubali wataka sifa wanaotafuta vyeo eti kwa kuonesha wanaonea wapinzani wafanye hivyo Tarime.
Tarime hatujawahi kuwa waoga tutasimama imara na tutashinda kwasababu tuko kwenye haki.