Kocha maarufu nchini Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema mafanikio aliyonayo leo Mbwana Samatta yametokana na muono wake wa mbali na kutolewa sifa pamoja na kuridhika kwa mafanikio madogo ambayo alianza kuyapata mapema.
Julio amesimulia mkasa mmoja ambao unathibitisha mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji hakulewa mafaniko badala yake alikuwa anapambana ili kufika mbali zaidi.
“Siku moja tulikuwa Cameroon au Nigeria, Samatta na Ulimwengu walikuwa wamekaa chumba kimoja, ikafika muda wa kwenda shopping huwa inatokea siku mmoja kabla ya mechi, Samatta na Ulimwengu walivyofatwa na meneja wakakataa,” anasema Julio ambaye wakati huo alikua kwenye benchi la ufundi la timu za taifa.
“Mimi nikakasirika nikawafata na kuwauliza kwa nini mnakataa? Ni kwa ustaa gani mliokuwanao? Samatta akaniomba radhi akasema alimwambia meneja aondoke kwa sababu wao hawataenda kwenye shooping.”
“Nikaondoka zangu nikiwa bado nimekasirika, tukaenda madukani tukarudi siku iliyofata tukacheza mechi tukamaliza, jioni Samatta akanifata akaniambia mwalimu samani kuna jambo nataka kukwambia, wakati wa kununua raba na ma-jeans haujafika kwasababu hela yenyewe haitoshi wakati huo bado baba, girlfriend, wanataka hapohapo bora hiki kiasi kidogo tunachopata tukiweke ukiokota-okota unaweza kununua hata kiwanja lakini muda wa kununua raba na jeans utafika tu, nikamuelewa sana,” anasema Julio.
“Siku moja nikakutana nae airport mimi nikiwa nawasindikiza wanangu yeye alikua anaondoka, akaniuliza mwalimu unakumbuka? Kuna kipindi nilikwambia wakati wa kununua jeans na raba haujafika, sasa hivi wakati umefika ninaweza kununua raba hata kwa dola za Marekani 500, nikampa mkono nikam-hug nikasema huyu alikuwa na vision.”
“Mimi nilenda Shinyanga watu wakaanza kusema Julio na ujanja wake wote ameenda kukaa shamba lakini walikuwa hawajui mimi nimefata nini kule, nimekaa Shinyanga leo nina mbuzi na ng’ombe nimenunua nikiwa Shinyanga.”
Kwa sasa Julio ameweka pembeni ukocha kutokana na kutoridhishwa na baadhi ya waamuzi huku akitajwa kupewa deal katika klabu ya Simba japo bado haijatangazwa rasmi.