Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), Mike Pompeo kesho alhamisi ya Februari 9, 2017 anataraji kufanya ziara ya nchini Uturuki ambapo akiwa nchini atafanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Serikali ya Uturuki imesema mazungumzo ya Pompeo na Erdogan yatakuwa yamejikita zaidi kuzungumza kuhusu usalama wa Uturuki katika juhudi zao za kupambana na makundi kigaidi.
Ziara hiyo ya Pompeo imekuja ikiwa ni baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kufanya mazungumzo ya simu kwa dakika 45 ambapo mazungumzo hayo yalilenga uhusiano wa mataifa hayo na jinsi Marekani inavyoweza kuisaidia Uturuki kuimarisha usalama.
Taarifa ya Ikulu ya White House ilisema kuwa mazungumzo ya viongozi hao wawili yalilenga jinsi Marekani itashirikiana na Uturuki jinsi ya kupambana na ISIS hivyo ziara ya Pompeo inatizamiwa kujadili usalama lakini zaidi kuhusu jitihada za Uturuki kupambana na ISIS.