Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO) umzindua kozi ya wiki tano kwa wanajeshi wa Iraq kwa ajili ya kuwafunza jinsi ya kutegua mabomu ambayo yanakuwa yametengwa na maadui.
Katika taarifa ambayo imetolewa na NATO imeeleza kuwa lengo la kozi hiyo ni kuwafundiswa wanajeshi ili waweze kutegemea mabomu ambayo yanafishwa na wanamgambo wa makundi mbalimbali ya kigaidi ikiwepo Islamic State yanayotega mabomu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Akizungumza kuhusu kozi hiyo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alisema mafunzo hayo yatahusisha wanajeshi 30 ambao watafunzwa kikamilifu jinsi wanavyoweza kutegua mabomu ili waweze kupambana na makundi ya kigaidi.
“Mafunzo ya NATO ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanajeshi wa Iraq 8ili wawe na uwezo wa kupambana na ISIL na kwa ajili ya usalama wao wenyewe,
“Silaha pekee tuliyonayo ya kupambana na ugaidi ni kutoa mafunzo kwa majeshi ya eneo husika … kama jeshi la Iraq likipambana kwa ufanisi basi Iraq itakuwa salama na zaidi kwa nchi za Mashariki ya Kati,” alisema Stoltenberg.