Mitandao ya Sudan Kusini inamuonyesha Rubani Mtanzania aliyekuwa "ametekwa" huko Juba kutokana na ugomvi wa upande mmoja na Serikali iliyopo madarakani.Ikihisiwa kuwa Tanzania ipo nyuma ya ugomvi wa pande mbili za mahasimu wa nchi hiyo.
Kutekwa kwa rubani huyo,kulichagizwa zaidi na ujio wa mke wa Garang na ujumbe wake kwa Rais John Pombe Magufuri,ukiambatana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa nchi hiyo Ndugu Garang Mabior de Garang.
Kwa "udadisi" wa picha hiyo,anayeonekana bila shaka ni Captain Mazrui,mmiliki wa kampuni ya Zenith Aviation yenye makazi yake Zanzibar.Ndege iliyokamatwa ni aina ya C208 yenye usajili wa 5H-MZA ambao ni wa Tanzania.
Kukamatwa na hadi kuachiwa kwake ni kama pamekuwa "kimyakimya".Tungojee tamko la Serikali juu ya kukamatwa na hadi kuachiwa kwa rubani huyu.(Na uhakika wa Rubani).Kwani hata vyombo vya habari vya Sudani Kusini vinasema rubani huyo hana mawasiliano na wanaserikali huko Juba.
Captain Mohammed Nassor Saul (Mazrui) anamiliki kampuni hiyo ambayo hufanya huduma ya ndege za kukodi toka Zanz-Dsm,Znz to Mafia na Znz to Mombasa,yawezekana safari yake kwenda Sudan Kusini ilikuwa ni ya kukodiwa kibiashara kwa ndege yake.