Ikiwa leo ni siku ya pili kwa mwaka huu mpya wa 2017 yaani January 2 mwaka 2017 ni mwaka mpya kabisa ambao tumeuanza hapo jana ikiwa wengi wamewekeza matumaini yao ya kimaendeleo na mafanikio kwa mwaka huu ikiwa ilishindikana katika mwaka uliomalizika hapo juzi 2016.
Kama ilivyo kawaida ni wengi ambao wametumiana salamu za heri ya mwaka mpya na mengineyo katika suala zima la kutakiana amani na furaha katika mwaka huu mpya ambao tumeuanza. Hata mastaa wetu wa hapa Bongo hawakubaki nyuma katika suala hilo la kutakiana heri ya mwaka mpya. Madee ni mmoja kati ya mastaa ambao walizitumia pages zao za Instagram katika kutakiana heri ya mwaka mpya.
Itakuacha mdomo wazi post ya Madee katika kurasa yake ya Instagram baada ya kupost picha ambayo inamuonyesha akiwa analia na kuandika maneno yenye kumgusa kila mmoja katika hali ya kibinadamu, ikiwa yanahusiana na mengi ambayo yametokea katika mwaka 2016, mazuri na hata mabaya.
Chukua muda wako kuisoma hii post hapa chini kisha niachie comment yako ukiniambia ni kipi ulikiwaza kabla ya kumaliza kuisoma post hii.