Unene ni hali ya kuongezeka upana wa mwili na uzito kwa kasi.
Upana huu huongezeka katika maeneo yote ya mwili chini ya ngozi na kusababisha mrundikano wa mafuta maeneo yanayohusiana na kuongezeka kwa mwili au kuonyesha mtu amenenepa kutofautiana kati ya mwanaume na mwanamke, lakini tofauti hii siyo kubwa.
Kwa ujumla mtu anayenenepa hupatwa na matatizo mengi, kubwa ni kushindwa kuumudu mwili na madhara mengine katika mfumo wa upumuaji na uzazi.
Tatizo pia huweza kutokea katika mfumo wa chakula, kuwa na hamu sana ya kula na katika mfumo wa mifupa hupatwa na matatizo mbalimbali ya maumivu ya mifupa au ganzi.
Kuna tofauti kidogo kati ya unene na kuongezeka uzito. Kwa kawaida uzito wa mwili hutokana na mifupa kwa kiasi kikubwa, mtu anaweza kuongezeka uzito sanjari na kuongezeka urefu na mwili, hii hasa kwa watoto na vijana lakini kwa mtu mzima au kijana kuanzia umri wa miaka ishirini na tano hatutegemei urefu unaweza kuongezeka, mara nyingi umri huu ni wa kuanza kunenepa.
Ukuaji wa mwili kama tulivyoona ni kuongezeka urefu na uzito, hali hii inategemea na asili ya vinasaba katika ukoo wenu.Ukuaji huishia kipindi cha balehe kwa mvulana na msichana katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu tangu avunje ungo.
Ukuaji wa kasi unatokea kama mtoto atakuwa anakula chakula vizuri na mwili wake unapata mazoezi ya kutosha na anakuwa na afya njema pasipo kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara.
DALILI ZA KUNENEPA
Kunenepa kunapoanza, unaweza usijijue, unaona nguo zinaanza kukubana, unahema harakaharaka unapotembea umbali mfupi au kupandisha ngazi.
Kunenepa kunapoanza, unaweza usijijue, unaona nguo zinaanza kukubana, unahema harakaharaka unapotembea umbali mfupi au kupandisha ngazi.
Mashavu yanaongezeka na nyama uzembe zinaanza kujaa mbavuni na kifuani.
Tumbo linakuwa kubwa (kitambi) na hii ni kwa wote, wanaume na wanawake. Wanawake wengi sasa hivi wameanza kuwa na vitambi na wengi huwa na matumbo makubwa hasa baada ya kujifungua.
Kwa wanawake nyama uzembe hujaa pia mabegani na katika makalio na mapajani kwa ndani katika maeneo ya sehemu za siri.
Mtu mnene hulalamika maumivu ya kiuno, magoti na wengi hushindwa kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi. Kwa mwanaume sehemu zake za siri huonekana ndogo kutokana na mafuta kujaa eneo husika.
NINI CHA KUFANYA?
Unene ni mrundikano wa mafuta chini ya ngozi, kinachotakiwa ni kuyaondoa mafuta hayo. Zipo njia nyingi za taratibu na za haraka za kuondoa mafuta hayo na nyama uzembe.
Njia za taratibu ni kufanya mazoezi na kudhibiti vyakula. Epuka kukaa au kushinda bila kula. Njia ya pili na ya haraka ni kutumia dawa zinazoyeyusha mafuta, kudhibiti hamu ya kula huku ukifanya mazoezi mepesi.
Dawa zipo za aina nyingi, lakini hakikisha unatumia dawa nzuri zisizo na madhara wala usumbufu kwa kuwasiliana na daktari wako.Dawa hizi huondoa mafuta ya ziada chini ya ngozi na nyama uzembe na ukifanya mazoezi, mabadiliko unayapata kwa haraka sana kwa takriban siku tisa na huwa zina gharama kubwa kiasi.
Mpangilio wa vyakula huzuia uzalishaji wa tabaka la mafuta au kudhibiti lililopo lisiendelee hasa wakati unatumia dawa au kufanya mazoezi.Madhara ya unene ni kupata magonjwa ya ngozi hasa sehemu za nyama zilizojikunja, mfumo wa hewa kuwa wa kubanwa na kifua, kikohozi cha mara kwa mara, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, magonjwa ya kisukari, misuli na mifupa.
Mwanamke kuchelewa kushika ujauzito na kupata matatizo katika kizazi na vifuko vya mayai, kwa mwanaume hupungukiwa na nguvu za kiume na kuchoka sana baada ya kumaliza tendo la ndoa.