Kama kawaida mpira pesa na sio misifa, kila hatua ni biashara kwa wachezaji wa kwenye ligi kubwa. Wayne Rooney amefunika hadi habari ya matokeo ya 1-1 dhidi ya Stoke, habari ya kuwa mfungaji bora wa muda wa Manchester Unites ndio imekua kubwa.
Mara baada ya kutupia goli la 250, Nike ambao ni wadhamini wa Rooney kwenye viatu. Wametangaza kutoa kiatu maalum WR250 kusherekea rekodi hiyo mpya. Tamko la Nike lilikua hivi, “Leo Wayne Rooney amekua mfungaji bora wa club ya kwa muda wote baada ya kufikisha goli la 250. Rooney amefanikisha rekodi hii ndani ya miaka 12 ambayo ni haraka miaka 5 zaidi ya aliyekua anashilikia rekodi hii hapo zamani. Kusherekea rekodi hii Nike Football inatamburisha kiatu maalum toleo ya Hypervenom WR250”
Kiatu hicho kina rangi ambazo Rooney amevaa kwa muda mrefu pamoja na lgo maalum yenye namba 250. Kama kawaida mauzo ya kiatu hiki yanachangia pato la Wayne Rooney.