Halmashauri ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22 na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango wa mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya barabara ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini.
"Katika uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla."
Aidha meya ametaja barabara ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.25, Viwandani km 1.68 na Tanesko soko la samaki ambazo zitajengwa ndani ya mwaka mmoja na kwa kiwango cha juu.
Kwa upande wake mkandarasi kutoka Estim Construction Jagdish Bhudia amesema kuwa watajenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa kama kwa kutumia lami nzito ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.
Hata hivyo mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni ameongeza kwa kuwataka wanachi wote wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huu ambao unalenga kuboresha miundombinu na kuimarisha huduma za kiuchumi, kibiashara na kijamii.
Na Amina Kibwana,Globu ya jamii