Kila mtu anajua kwamba Wenger na Mourinho hawapatani kwa muda mrefu sana kutokana na maneno walikua wanatupiana. Lakini kabla ya mechi ni kitendo cha kiungwana kupeana mikono kwa managers.
Siku ya leo Jose na Arsene wapeana mikono kiukavu sana kiasi kwamba hakuna hata mmoja kati yao alimpa mkono mwenzake kwa kumuangalia sura. Kila mmoja aliangalia upande mwingine akiwa anampa mkono. Hizi ni picha 3 wakipeana mikono.


