SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Novemba 2016

T media news

LADY JAY DEE AZUA MJADALA MITANDONI KUHUSU KINACHOZANIWA KUWA AMEFUNGA NDOA KIMYA KIMYA NIGERIA NA MSANII WA LEBAL YA MR FLAVOUE, SPICY


Miongozi mwa picha zilizozua mjadala kwenye mitandao ya mijamii ni pamoja na hiyo juu ya Jay dee akiwa na Msanii Spicy anayefanya kazi kwenye lebel ya Mr Favour nchini nigeria.


kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha wa instragram  watu wa karibu na msanii jay dee wamekuwa wakituma jumbe za pongezi kitu ambacho kinatoa tafsiri kuwa ameingia kwenye maisha mapya.



 

meneja wake aliulizwa na moja ya mtandao hapa tanzania alijibu kwa mkato tu kuwa jay dee ni sawa na wao akimaanisha kuwa ameingia mbilini ingawa yeye mwenyewe hakutoa taarifa rasmi.

Kwenye post moja akiwa naye, Spicy ameandika: Can’t really explain it… So into you.” Kwenye nyingine ameandika: Don’t get it twisted, love is a beautiful feeling.” Siku kadhaa zilizopita, Jide alipost picha ya Spicy na kuandika: Wanna follow my bae???I permit you 





 Follow him now @spicymuzik.”

Post zao zinazidi kuipa nguvu imani ya wengi kuwa huenda ikawa kweli Jaydee ameanguka kwenye penzi la staa wa Nigeria.

Lakini hebu tukeche akili kidogo. Kwanza, si kila unachokiona kwenye Instagram au mitandao mingine ya kijamii ni kweli – tena inapomhusu mwanamuziki! Vipi kama ikiwa ni video ya muziki? Mheshimiwa Temba (ana mke tayari), Linex, Akothee na wasanii wengine wamewahi kutuaminisha kuwa wamefunga ndoa lakini baadaye ikaja kuwa ni video ya muziki.

Kingine, tangu nimeanza kumfahamu Lady Jaydee, sijawahi kumtambua kama mtu anayeweka hadharani mambo yake binafsi. Hiyo ni ‘rule’ kubwa aliyojijengea kwa muda wote wa career yake – ana usiri wa hali ya juu katika mambo ya uhusiano. Na ndio maana hata wakati akiwa mke wa Gardiner G Habash, maswali ya ndoa yake alikuwa hayapi nafasi. Iweje leo Jide amekuwa mtu wa kuweka sana mahusiano yake mtandaoni? Umelifikiria hilo?

La mwisho, wiki moja iliyopita ambayo Jide na Spicy walikuwa visiwani Zanzibar, ndio wiki ambayo muongozaji wa video wa Afrika Kusini, Justin Campos na mke wake Candice, walikuwa huko.