SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

T media news

Wachezaji 9 wenye majina magumu kuyatamka

Kuna baadhi ya wachezaji majina yao yamekuwa ni changamoto kwa wadau wa soka hasa pale wanapotaka kuyataja, changamoto hii inatokana na urefu wa majina hayo au ugumu wa majina yenyewe.

Kwa upande wa Tanzania inawezekana Kiswahili pia kinasababisha tupate changamoto ya kuyataja baadhi ya majina. Mfano, lugha ya Kiswali neno husomwa/kutamkwa kama linavyoandikwa, lakini katika lugha nyingine hakuna uhusiano kati ya neno linavyoandikwa na linavyotamkwa.

Mfano mdogo ni namna ya jina la timu ya Crystal Palace ya England inavyoandikwa na inavyotamkwa, watanzania wengi tunatamka ‘kraisto’ badala ya ‘kristo’.

Hapa nimekuletea orodha ya majina 9 ya wacheza soka ambayo huenda yakawa ni changamoto kwa baadhi ya wadau namna ya kuyatamka kutokana na urefu wa majina hayo au ugumu wa kuyatamka kwa usahihi.

9. Diniyar Bilyaletdinov

8. Jan Vennegoor of Hesselink

7. Alex Oxlade-Chamberlain

6. Lazaros Christodoulopoulos

5. Jakub Błaszczykowski

4. Reza Ghoochannejhad

3. Cameron Borthwick-Jackson

2. Sokratis Papastathopoulos

Mohamed Lamine Zemmamouche