SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 30 Septemba 2016

T media news

Shabiki wa Simba aeleza alivyopelekwa polisi kwa kushangilia kufungwa kwa Yanga

Bi Halima ambaye ni mwanachama wa klabu ya Simba kwa sasa anamiaka 76 alipiga story na Sports Extra ya Clouds FM na kuelezea baadhi ya mambo ya kishabiki enzi hizo kuelekea game ya Simba na Yanga.

“Mimi nilikuwa napata furaha tu na nilikuwa najiamni na timu yangu ya Sunderland, Yanga tulishaifunga mara nyingi mapa ikawa inaitwa ‘four, four’ kwasababu ya vipigo vya magoli manne mfululizo.”

Kitu gani kigumu ambacho umewahi kupitia katika mechi za Simba na Yanga?

“Nilishapelekwa polisi kwasababu ya kushangilia kufungwa kwa Yanga mwaka 1976 walivyocheza na Inugu Rangers, mimi nikawa nashangilia Inugu Rangers kwa nguvu zangu zote, wakaja kunichukua wakanipeleka polisi wakati huo nilikuwa nakaa mtaa wa Udowe.”

“Tulipofika kituoni, yule mzee aliyenikamata kunipeleka polisi kumbe si mwanachama wa Yanga, tulikuwa tumekaa na mkuu wa kituo kwenye baraza la usuluhishi akaniuliza wewe ni mwanachama wa Simba nikasema ndiyo nikaonesha kadi yangu ya Simba, yule mzee kadi hana basi mkuu wa kituo akamwambia yule mzee hana haki ya kunishitaki kwasababu yeye si mwanachama ni shabiki tu.

Kwahiyo haya mambo ya Simba ikicheza mechi ya kimataifa na timu nyingine, halafu watu wanashangilia timu nyingine kumbe imeanza zamani?

“Imeanza zamani sana, Simba ilicheza na waarabu hapa mwaka 1974 ikafungwa, Yanga walishangilia hadi mwisho. Mwaka 1975 Yanga nao wakacheza na waarabu kwao wakafungwa goli tano ndio mwaka ambao ilianza kutumika shilingi tano ‘dala’ ikawa ukisema dala Yanga wanakutukana wakidhani unawatania.”

“Miaka ya nyuma Simba na Yanga zilikuwa zinakutana mara moja kwa mwaka, ushabiki ulikuwa juu sana, wiki mbili kabla ya mechi shabiki wa Simba hapiti Yanga na shabiki wa Yanga hapiti Simba. Sikuhizi ushabiki umekufa kwasababu Simba na Yanga zinacheza mechi nyingi inafika wakati hadi zinacheza mechi za kirafiki.”