Mwathiriwa wa dhuluma. Visa vya dhuluma za kimapenzi dhidi ya watoto vimekuwa vikiongezeka nchini Kenya licha ya adhabu kali inayotolewa kwa wakosaji.
Mwathiriwa wa dhuluma. Visa vya dhuluma za kimapenzi dhidi ya watoto vimekuwa vikiongezeka nchini Kenya licha ya adhabu kali inayotolewa kwa wakosaji.
Msichana mdogo mwenye umri wa miaka 15 mjini Maua adaiwa kunywa dawa ya kuua vijidudu shambani baada ya kusemekana kubakwa
– Msichana huyo anapata afueni katika hospitali moja mjini Maua
Msichana mdogo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea kupata afueni katika hospitali moja mjini Meru baada ya kujaribu kujitia kitanzi kwa kile kinachosemekana kuwa alinajisiwa na mjomba wake.
Inasemekana kuwa msichana huyo alikunywa dawa ya kuua vijidudu shambani kufuatia kitendo hicho katili na mtu aliyestahili kuwa mlezi wake.
Binti huyo alipatikana amezirai na kukimbizwa katika hospitaali ya Mau Methodist anakoendelea kupata afueni.
Msichana huyo alisema kuwa, alirejea nyumbani na kupata wajomba wake wawili pamoja na shangazi.
Mjomba mmoja akaondoka na shangazi yake huku mwingine akisalia. Binti huyo akachukua chakula kwenda kula nje lakini mhusika aliingia nyumbani kwake na kutwaa upanga.
Wanawake mjini Nyeri walivizia genge la wabakaji katika kijiji kimoja na kunasa mshukiwa mmoja. Nusura mshukiwa huyo aangamizwe na umati uliokuwa na hasira.
Mwathiriwa wa ubakaji.
Mjomba huyo kisha akamwita ndani na kumuagiza avue nguo zote na kulala kwenye kiti.
“Niliingia ndani ya nyumba kama nilivyoagizwa na nilipofika alikokuwa aliniagiza kuvua nguo na kulala kwenye kiti ambapo alininajisi mara kadha,” msichana huyo alisema kama alivyonukuliwa na Nairobi News.
Mjomba alimnajisi na kisha kumuagiza kuondoka.
Msichana huyo aliapa kuwa kamwe hatarejea nymbani kwa nyanyake na anataka haki kutendeka.
“Siwezi kuvumulia kumuona mjomba huyo aliyenitendea haya. Afadhali nife kuliko kumuona na kukumbuka kila mara aliyonitendea,” msichana huyo aliongeza.
Visa vya ubakaji na unajisi vimekuwa vikiongezeka nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni.
Serikali imehimizwa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wabakaji ili kudhibiti visa hivyo.


