Na Alfa Chapalama
Nimefanya utafiti mdogo kuhusu namna hizi club tatu za Tanzania AZAM, SIMBA NA YANGA, jinsi zinavyotumia tovuti zao, nimebaini kuwa kuna tatizo hasa katika upande wa maafisa habari wa club hizi mbili yani SIMBA na YANGA, tofauti kidogo na AZAM.
Katika tovuti ya Yanga utashangaa kuona bado kuna taarifa za muda mrefu uliopita, wakati Yanga imepitia katika mambo mengi mapya mazuri hivi karibuni lakni hakuna kilichowekwa humo, yani utastaajabu kukuta bado kuna habari za JAJA wakati Yanga saizi inawachezaji wanaotikisa na gumzo kama kina Kamusoko, Ngoma, Bosou, Mahadh nk.
Hakuna story yoyote kuhusu mashindano haya ya CAF Confederation Cup hasa katika hatua hii iliyofikia.
katika tovuti ya Simba ndio kicheko zaidi, yani humo ndio wana story ambazo hata haieleweki za lini, story ya mwisho kwenye website ya Simba inamhusu Haruna Moshi ‘Boban’.
Angalau kidogo Azam FC kuna story zinzzokwenda na wakati.
Kilichonishtua kuandika hili ni baada ya kukuta story ya Ngoma kwenye tovuti ya CAF ya tare 11-8-2016, nikajiuliza, yani CAF wanaandika kuhusu Ngoma huku wenye mchezaji bado wana story ya Jaja? Hapo ndipo nikafahamu kwanini yule tajiri anataka kukodi Yanga? na yule mwingine kutaka hisa nyingi Simba.
Klabu zetu hazijiendeshi kiuweledi, ndiyo maana hata Yanga imeshindwa kufanya usajili kwa njia ya mtandao mapema mpaka kupelekea muda kupita, huku wakisingizia mtandao ulikuwa down, yani wamezidiwa mpaka na Ndanda FC ya Mtwara.
Halafu eti timu zetu zinataka kuwa kama TP Mazembe wakati hao mazembe ukienda kwenye tovuti yao, iko bize muda wote wana-update habari kuhusu klabu yao, ratiba za mechi na matukio mengine yanayohusu wachezaji wao. Hizi timu zinapaswa kubadilika ili zijiendeshe kiuweledi kwa kuzingatia fursa za tecnolojia tuliyonayo.
0714073333