SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 8 Agosti 2016

T media news

VIGOGO WAUZA 'UNGA' SASA KUKIONA CHA MOTO,MWIGULU AWASHA MOTO

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa wa Songwe, kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.

Nchemba alitoa agizo hilo jana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo alisema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na dawa za kulevya.

Alisema kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani, wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.

“Hatuwezi kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania. Hili linatuchafua sana,” alisema Nchemba.

Aliutaja mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako