SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

T media news

MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA MKUTANO USIYO RASMI SOKO LA MWANJELWA



 

-APokelewa na kilio cha wafanyabiashara wadogo kuomba serikali iwapeleke wafanyabiashara wenzao ktk masoko rasmi

Wampongeza kwa kuwajali na kuwasaidia kupunguziwa kodi na ushuru

Amwagiza Dc na mkurugenzi kwa Simu watoe ilani YA siku 7 wafanyabiashara kwenda masoko YA sido, Soweto na mwanjelwa. Amwambia barua ataipata ndani YA saa moja

Uamuzi huu utasaidia kuweka jiji safi, ushindani Sawa na utaongeza mapato


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika hali isiyo YA kawaida akiwa katika Duka la Voda shop lililopo soko la mwanjelwa alisimama Sauti za akinamama " Njoo baba, njoo huku utusikilize baba na akaamua kuwasogelea na kuingia sokoni na ndipo umati ukamzingira kumfikishia kilio cha kumuomba kwa Mamlaka aliyonayo aamuru wafanyabiashara wenzao warejee katika masoko rasmi kwani wao hapo walipo hawana biashara wanalipa ushuru na Biashara ktk masoko ni ngumu kwasababu wenzao waliopo Kabwe na kwenye maeneo yaliyokatazwa hawalipi ushuru na zaidi wanapanga biashara maeneo hatarishi 

Akiwa eneo la Tukio alimpigia Mkuu wa wilaya Simu na kumwagiza tarehe 9 siku ya Jumanne atoe ilani na awape siku saba wafanyabiashara wote wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi na kwenye road reserve waondoke wenyewe na waende kwenye masoko YA mwanjelwa , sido na Soweto 

Amesema mkakati wa serikali ni uliweka jiji la Mbeya katika hali YA usafi ameanza na kuyaondoa malori YA mizigo na ku yatapitia eneo maalum sasa operesheni ni kuwaondoa wanaofanya biashara manei yasiyo rasmi na kwenda masoko rasmi

Aidha wafanyabiashara hao wamepongeza Mkuu wa Mkoa mara alipoteuliwa na kuripoti amewafanyia jambo kubwa sana wafanyabiashara hao kwa kupunguza kodi YA vyumba kutoka sh laki tano hadi laki 250 kwa vyumba vya juu , kutoka laki 5 hadi laki 350 kwa vyumba vya chini na kupunguza ushuru wa vizimba kutoka sh 3000 hadi shilingi Mia tano

Pia wamepongeza ujasiri wa kuunda tume ya kuchunguza ujenzi wa soko na taratibu za upangishaji soko la mwanjelwa