SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 9 Agosti 2016

T media news

MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI ESTER AMOS BULAYA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KWA WANANCHI WA BUNDA MJINI.*


-------------------------------------------
Leo majira ya saa 5:00 asubuhi ndani ya viwanja vya *saba saba* mjini Bunda mhe. ESTER AMOS BULAYA MBUNGE wa JIMBO LA BUNDA MJINI ameanza kutekeleza ahadi alizohaidi wakati wa kampeni.

Mojawapo ya ahadi zake ni pamoja na kuwawezesha VIJANA kushiriki kikamilifu katika michezo, limejidhihilisha hilo leo baada ya mhe. MBUNGE kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya tsh milioni kumi na mbili *12,000,000/=*

Mhe. MBUNGE amekabidhi vifaa hivyo kwa timu *49* yaani kila timu ya mtaa na kijiji kwaajili ya maandalizi ya *ESTER CUP* mapema mwezi *October 2016.*

Ikumbukwe kuwa fedha hizo ni fedha kutoka mfukoni mwa MBUNGE mwenyewe yaani kupitia mshahara wake na si vinginevyo.

Wakizungumza Mara baada ya kukabidhiwa jezi na mipira VIJANA hao wamemshukru mhe. MBUNGE kwa kusema kuwa ni MBUNGE wa kwanza Tanzania ambae ameweza kutoa fedha yake mfukoni tena yenye thamani kubwa kiasi tajwa hapo juu na kuwapa vijana.
*HAKIKA TUKO PAMOJA NAWE NA TUTAENDELEA KUWA PAMOJA DAIMA*

Aidha mhe. MBUNGE pia ametumia fursa hiyo kutekeleza ahadi yake kwa VIJANA wa BODA BODA kwa kuwachangia pikipiki mbili zenye thamani ya tsh milioni nne *4,000,000/=* kupitia kikundi chao cha *ULIPO TUPO* za kuanzia na baadae wataongezwa nyingine nne.

Pia wakati wa kampeni mhe. MBUNGE alihaidi kuhakikisha zinaanzishwa *SACCOS* za Kata kwa kulitekeleza hilo leo mhe. Mbunge amezindua *SACCOS* mbili ambazo ni *Nyasura SACCOS* na *furahisha SACCOS kitaramaka* na hatimae kuwachangia tsh milioni moja *1,000,000/=* kwa kila *SACCOS*

Sambamba na hayo yote mhe. Mbunge ametenga tsh milioni kumi na tano *15,000,000/=* kwaajili ya vikundi ambapo anaendelea kutoa *motisha* kwenye vikundi wakati wakisubili fedha za *5%* toka halmashauri.


Imetolewa na:-

*KAUNYA YOHANA*
*KATIBU WA MBUNGE*
*JIMBO LA BUNDA MJINI*