SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 17 Agosti 2016

T media news

MAMBO MATANO AMBAYO YANAFANYA UBINGWA KWA ARSENAL KUWA NDOTO MSIMU HUU

Ni ukweli uliodhahiri kwamba washabiki wengi wa Arsenal wanafahamu fika kwamba chini ya utawala wa Arsene Wenger hakuna kitakachobadilika kutokana na kupata matokeo ya aina hiyo hiyo kila uingiapo msimu mpya.

Mara zote kuelekea mwishoni mwa msimu, maumivu huwa makubwa zaidi kutokana na timu yao kuishia kuwania nafasi ya kucheza Michuano ya Uefa Champions League, na si ubingwa kama ambavyo wapinzani wao hupambana kupata.  Msimu huu mambo yameanza mapema tena baada ya kufungwa nyumbani kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Liverpool, licha ya msimu uliopita kufanyiwa hivyo pia na West Ham.

Sasa hapa tumekuwekea mamb matabo ambayo hayawezi kutoa mwanga wowote kwa Arsenal kutwaa ubingwa.

Kupoteza mchezo wa ufunguzi

Kupoteza mchezo wa ufunguzi uliopigwa Jumapili dhidi ya Liverpool kunaongeza hofu. Ni mwaka wa tatu kati ya miaka minne sasa Arsenal hawajaanza vizuri mechi za ufunguzi wanazocheza nyumbani. Walianza na Aston Villa mwaka 2013 wakapigwa 3-1, wakaja na West Ham msimu uliopita wakala 2-0, na msimu huu wamechezea 4-3 kutoka kwa Liverpool.

Kimsingi, Arsenal wameshinda mara moja tu kwenye mchezo wao wa ufunguzi ndani ya miaka saba. Waliwafunga Crystal Palace 2-1 mwaka 2014. Ni toafauti sana na rekodi ambayo Wenger aliiweka kati ya mwaka 2001-2009, wakati Arsenal waliposhinda michezo nane ya ufunguzi na kutoka sare mmoja dhidi ya Aston Villa mwaka 2006. Hii inaleta mshangao mkubwa kwamba ni vipi kwenye miaka ya hivi karibuni, Arsene Wenger amekuwa haandai timu kikamilifu kwaajili ya michezo ya ufunguzi.

 

Kukosekana kwa usajili mpya

Arsenal wanarudi kule kule kwa miaka yote kutokana na kuhusishwa na usajili wa wachzaji kibao lakini pasipo mafanikio. Miaka ya hivi karibuni wamewahi kuhusishwa na usajili wa wachezaji kama Gonzalo Higuain, Luis Suarez ns Karim Benzema lakini wote hao ilishindikana kuja. Safari hii mwanzoni tuliona akiwapa moyo mashabiki wa Arsenal baada ya kufanya usajili wa mapema kabisa huku akiahidi kuleta wachezaji wengine kama beki wa kati na mshambuliaji. Lakini tumeshuhudia wapinzani wake wakifanya hivyo na yeye akiishia kuongea tu mpaka sasa hakuna alichokifanya.

Wakati huu ambao kuna tetesi za usajili wa beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi, hakuna dalili yoyote kama kuna uwezekano wa kusajiliwa mshambuliaji mpya klabuni hapo.

Huu ni msimu wa tatu ndani ya miaka minne ambapo Arsenal wameanza ligi bila ya kuwa wamefanya usajili wa maana. Mwaka 2013, Wenger hakuwa amefanya usajili wowote mpaka siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili akamleta Mesut Ozil. Msimu uliopita akajipiga akamleta Petr Cech pekee na wala hakuhangaika na mshambuliaji ilhali anajua fika timu yake inahitaji straika.

Kweli inawezekana kwa tabia za hivi karibuni za Wenger kufanya usajili siku za mwisho kabla ya dirisha kufungwa, bado ana nafasi ya kuanya usajili, lakini hii haiondoi uhalisia kwamba biashara nzuri hufanyika mapema na sio mpaka maji yafike shingoni.

Mshabiki kuzomea baada ya mchezo dhidi ya Liverpool

Baada ya mchezo wao dhidi ya Liverpool kumalizika zilisikika sauti za mashabiki wa Arsenal zikizomea kutokana na matokeo mabovu ya timu yao nyumbani.

Zilisikika sauti kutoka kwa mashabiki zikitaka Wenger atumie pesa kwaajili ya kuleta wachezaji wapya. Kwa hali hii ya washabiki kuichoka timu yao mapema, bila shaka hakutakuwa na sapoti kubwa kwenye uwanja wao wa nyumbani na hivyo kusababisha wachezaji kukosa morali na hatimaye timu kufanya vibaya.

Mkosi wa majeruhi

Kama kuna kitu ambacho kimeshindwa kudhibitiwa kwa wachezaji wa Arsenal, basi ni suala la majeraha. Mapema kabisa kwenye mcheza wa ufunguzi tumeona wachezaji wawili muhimu Alex Iwobi na Aaron Ramsey wakitolewa nje kutokana na majeraha waliyopata. Tayari kundi wachezaji wengine ambao wako nje wakiuguza majeraha kama vile mabeki Gabriel Paulista na Per Mertesacker. Sasa hivi ndiyo kwanza msimu unaanza, je, itakuajie itakapofika katikati mwa msimu au kuelekea mwishoni mwa msimu?

 

Kurudi kwa kishindo (The bounce-back)

Kama kuna msamiati ambao umekuwa mdomoni mwa Arsene Wenger basi ni huu wa kurudi kwa kishindo. Amekuwa akisema hivi misimu kadhaa sasa kila anapofungwa basi kisingizio ni ‘tutarudi kwa kishindo’. Ni kweli wachezaji wake kama Mesut Ozil, Laurent Koscielny na Olivier Giroud watakuwa katika mchezo ujao dhidi ya Leicester lakini ni ukweli usiopingika kwamba, Arsenal inahitaji kurudi kwa kishindo kwa kuongeza wachezaji wenye tija na sio kurudi kwa kishindo kwa kumtegema Giroud kama mshambuliaji namba moja.