SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 15 Agosti 2016

T media news

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA NA VIONGOZI MBALI MBALI WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWENYE MSIBA WA MZEE ABOUD JUMBE

 Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Aboud Jumbe likiwasili nyumbani kwa marehemu Migombani, Zanzibar

 Watoto, Ndugu, jamaa na Viongozi mbali mbali wakipokea mwili wa Marehemu Mzee Aboud Jumbe mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Migombani ,Zanzibar.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akishiriki dua maalum mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ,nyumbani kwa marehemu Migombani Zanzibar.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (katikati)akishiriki dua maalum kwenye msiba wa Mzee Aboud Jumbe nyumbani  kwa marehemu Migombani , Zanzibar wengine pichani ni Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Mwanamema Shein (kushoto) kulia ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa

Safari ya kwenda msikitini kuswaliwa