Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amesema mashabiki wa muziki hawajui kama kuna mahusiano ya kawaida kati ya msanii wa kike na wakiume.
Rapper huyo ambaye amefunga ndoa miezi michache iliyopita, aliwekwa kitimo kwenye kipindi cha Weekend Chart Show cha Clouds TV na kuzungumzia tetesi ya kutoka kimapenzi na mdogo wake AliKiba aitwae Zuu.
“Sisi wasanii pia tunakuwa na marafiki, binti unayemtaja (Zuu) aliwai kuwa rafiki yangu kwa sababu anapenda muziki,” alisema Roma. “Kwa hiyo alikuwa shabiki kama mashabiki wangu wengine, kwa hiyo mimi nawashkaji huwezi kuniwekea mipaka,”
Aliongeza,”Watu hawataki kuamini kwamba kuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume ambao unakuwa namipaka ya kishkaji, ndio maana tetesi zinakuwa nyingi kwamba Dayna kumbe ni washkaji tu. Mkikutana mnapiga seflie zinaenda uraiani, zikienda uraiani raia hawaamini kama kuna mahusiano ya kawaida kati ya msichana na mvulana, lakini hakuna kitu kingine sisi ni washkaji tu,”
Rapper huyo kutoka Tongwe Record kwa sasa anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Kaa Tayari’ akiwa amewashirikisha Jos Mtambo pamoja na Darassa.