Borussia Dortmund wamefanikiwa kumsajili winga wa Kijerumani Andre Schurrle kutoka kwa mahasimu wao klabu ya Wolfsburg kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
Schurrle (25) ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea amesaini mkataba wa miaka mitano kukipiga kunako wanjano hao.
“Ana uzoefu mkubwa sana katika soka la kimataifa na ubora wake utaisaidia sana timu yetu,” alisema Mkurugenzi wa Michezo wa Dortmund Michael Zorc.
Usajili huo umekuja siku chache baada ya Dortmund kmsajili tena mshambulizi wao wa zamani Mario Gotze kutoka Ujerumani.
Schurrle amefunga magoli 48 kwenye michezo 174 ya Bundesliga na amefunga magoli 20 kwenye michezo 55 katika timu ya taifa. Alikuwa ni sehemu ya kikosi kilichofika nusu fainali ya Euro mwaka huu ambacho kiling’olewa na Ufaransa.
Alijiunga na Wolfsburg Februari 2015 kwa ada ya paundi ml. 22 akitokea klabu ya Chelsea.