SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 3 Julai 2016

T media news

MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI AFICHUA JIPU LA KUTISHA


Ni jipu. Ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kusema halmashauri 34 nchini zimetumia Sh1.45 trilioni za miradi kugharimia shughuli ambazo hazikuwamo kwenye bajeti.
Profesa Assad ameyasema hayo katika mafunzo yaliyotolewa kwa watu wa kada mbalimbali kuhusu Toleo la Vijarida Maalumu vya Wananchi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni mwaka 2014 na kukusanya maoni ya ripoti ya CAG.
“Hili limekuwa tatizo kubwa hapa nchini. Utakuta fedha zimetengwa kwa mradi fulani, badala yake wanabadilisha matumizi na kununua vitu ambavyo havina stakabadhi,” amesema Profesa Assad.
“Lengo kuu la fedha hizo za miradi ni kutumika katika shughuli za maendeleo na kutoa huduma muhimu za kijamii.”