SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 26 Julai 2016

T media news

Ikulu Kubwa Zaidi Duniani



Je? Wajua kwamba Ikulu ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki aliyetaka kupinduliwa na wanajeshi wake ndiyo Ikulu kubwa zaidi duniani! Imegharimu pesa taslimu Euro milioni 400 kuijenga. Ukubwa wake ni mara thelathini ya ukubwa wa Ikulu ya Marekani maarufu kama White House.

Ikulu hiyo jengo lake linashangaza kwa ukubwa wake. Jengo hilo lipo katikati ya misitu ya Ataturk karibu na Jiji la Ankara. Eneo hilo lina ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 3000, likiwa na vyumba 1,150 pia lina vifaa maalum vya kuzuia mashambulizi yoyote yatakayoelekezwa kwenye jengo hilo.

Jengo hilo linafananishwa na himaya ya dikteta wa zamani wa Romania Nicolae Ceausescu kwa ukubwa wake. Jengo hili limepambwa na vito vya thamani kubwa. Gharama ya zulia la ndani pekee liligharimu Euro milioni 7.8, pia lina ngazi za umeme za kupandia juu ghorofani zipatazo 63. Pia sink za chooni moja imegharimu dola za Marekani 2,200 hadi 4,500 zikiwa zimepambwa kwa nakshi ya dhahabu.